Home Michezo BARCELONA YA MESSI YAPIGWA 8-2 NA BAYERN MUNICH NA KUTUPWA NJE LIGI...

BARCELONA YA MESSI YAPIGWA 8-2 NA BAYERN MUNICH NA KUTUPWA NJE LIGI YA MABINGWA

0

Nyota wa Barcelona, Lionel Messi akitoka Uwanja wa Luz Jijini Lisbon, Ureno kinyonge baada ya timu yake kuchapwa 8-2 na Bayern Munich katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa usiku wa Ijumaa hicho kikiwa kipigo kikubwa zaidi kwa vigogo hao wa Hispania tangu mwaka 1940.
Mabao ya FC Bayern Munich yamefungwa na Thomas Muller dakika ya nne na 31, Ivan Perisic dakika ya 21, Serge Gnabry dakika ya 27, Josh Kimmich dakika ya 63, Robert Lewandowski dakika ya 82 na Philippe Coutinho dakika ya 85 na 89, wakati ya Barcelona yamefungwa na David Alaba aliyejifunga dakika ya saba na Luis Suarez dakika ya 57.
Sasa Bayern Munich itakutana na mshindi kati ya Manchester City na Olympique Lyon zinazomenyana Jumamosi katika Nusu Fainali Agosti 19