Home Biashara Kampuni ya Bia ya Serengeti yazindua kampeni ya Serebuka

Kampuni ya Bia ya Serengeti yazindua kampeni ya Serebuka

0

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Mugisha (wa pili kushoto) akiongea na waandishi habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Serebuka inayolenga kuwafanya Watanzania kufurahia maisha kupitia bia ya Serengeti Lager na Serengeti Lite. Wa kwanza kushoto ni Lulu Kihwelo ambaye ni meneja wa mipango kwa wateja kutoka kampuni hiyo na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Bia Anitha Msangi.

Mtangazaji wa kituo cha redi cha Clouds FM Kennedy the Remedy  au Chui wa Facts (kushoto) akimuuliza swali mwandishi wa habari wa ITV Richard Stephen kabla ya kumpatia zawadi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Serebuka inayolenga kuwafanya  Watanzania kufurahia maisha kupitia bia ya Serengeti Lager na Serengeti Lite.

Waandishi wa habari wikifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Serebuka inayoendeshwa na kampuni ya Bia ya Serengeti ikilenga kuwafanya  Watanzania kufurahia maisha kupitia bia ya Serengeti Lager na Serengeti Lite.

Mkuu wa Kitengo cha Bia wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Anitha Msangi (kushoto) akionyeshwa orodha ya baadhi ya vyakula vinavyowezwa kupikwa kwa kutumia bia ya Serengeti lager na Upendo Mwalongo kutoka Open kitchen muda mfupi baada ya uzinduzi wa kampeni kubwa na ya aina yake inayojulikana kama Serebuka, inayolenga kuwafanya Watanzania kufurahia maisha kupitia bia ya Serengeti Lager na Serengeti Lite.

………………………………………

Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), leo imezindua kampeni mpya ya aina yake inayolenga kuwahamasisha Watanzania kufurahia maisha bila kikomo kupitia bidhaa zake zenye chapa ya Serengeti.

 Kampeni hiyo inayojulikana kama ‘SEREBUKA’ inadhaminiwa na chapa mbili maarufu, bia ya Serengeti maarufu kama  Serengeti Premium Lager na bia Serengeti Lite huku ikilenga kuonyesha kuwa Serengeti ni chapa inayowaleta Watanzania pamoja na kuwafanya wafurahia maisha bila kikomo.

 Kwa mujibu wa mkuu wa kitengo cha bia wa SBL Anitha Msangi, kampeni hiyo inakuja na mambo mazuri na ya kusisimua ikiwa ni pamoja na chakula, muziki na michezo.

 “Kampeni ya Serebuka ni kwa ajili ya Watanzania wote na inalenga kuwapa nafasi adhimu wateja wetu kufurahia maisha na bidhaa zetu zenye ubora wa kimataifa. Tutakuwa na mashindano ambayo yataongozwa na mastaa mbali mbali wataokuwa wanawaburudisha na kuwafurahisha wateja wetu katika kipindi chote cha kampeni,” anasema Anitha

 Mkuu huyo wa kitengo cha bia anasema kuwa, wateja wa Serengeti watakuwa na nafasi ya ‘Kuserebuka’ kwa kujirekodi wakishiriki kuimba, kucheza sebene maalum katika shindano la Serebuka asilimia mia na kuituma ambapo mshindi au kikundi cha washindi watashinda zawadi lukuki ikiwa ni fedha taslimu shilingi milioni moja. Wimbo wa Serebuka unaweza kupakuliwa kupitia mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, Mdundo. Watanzania watatakiwa kujirekodi kujishindanisha kwenye chalenji ya kuimba au kujishindanisha katika kucheza sebene kwa style yao wenyewe.

 Wateja pia kwa mara nyingine watamwona Chui wa Lite with a Bite katika tabia zake nne  na watapata nafasi ya kufurahia kuambatana nae kwenye matukio kwa kipindi chote cha miezi mitatu.

 “Kampeni ya Serebuka itawafikia wateja wetu Tanzania nzima kupitia baa zilizopo jirani yao na wateja wote wa chapa ya Serengeti wanasisitizwa kukaa tayari kufurahia maisha bila kikomo. Ili kushiri, tafadhali fuatilia #SerebukaAsilimiaMiaNaSerengetiLager na #SerebukaWithEveryBite,” Aliafafanua.

 Anitha aliwataka Watanzania kushiriki katika kampeni hiyo ya aina yake na kufurahia uhondo wa burudania tofauti tofauti kutoka SBL kupitia chapa zake zinazoongoza za Serengeti Premium Lager na Serengeti.

 Kampuni ya SBL ni mzalishaji wa kwanza wa wa bia yenye Kimea kwa asilimia 100, Serengeti Premium Lager na mzalishaji wa bia nyepesi iliyoasisiwa na kuzalishwa hapa Tanzania, Srengeti Lite. SBL pia ni wasambazaji wa pombe kali maarufu duniani kama Johnnie Walker, Ciroc,  Captain Morgan, Smirnoff vodka, White Horse, J&B na nyinginezo.