Home Mchanganyiko VIONGOZI MBALIMBALI WATEMBELEA MABANDA TAASISI ZA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO...

VIONGOZI MBALIMBALI WATEMBELEA MABANDA TAASISI ZA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO MKOANI SIMIYU

0

Aliyekuwa Katibu Tawala, Simiyu, Jumanne Sagini, akimsikiliza Afisa Uhusiano,
Salum Pazi, wakati akifafanua kuhusu shughuli za Mamlaka ya Udhibiti Udhibiti
Usafiri Ardhini (LATRA), wakati alipotembelea banda la mamlaka hiyo, Mkoani
Simiyu.


Kaimu Meneja Biashara na Masoko, Kampuni ya Usimamizi na Uendelezaji Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA, Azizi Jarufu akitoa maelezo ya aina ya mazao yanayosafirishwa kupitia kiwanja hicho kwa Aliyekuwa Katibu Tawala, Simiyu, Jumanne Sagini wakati alipotembelea bandala taasisi hiyo katika maonesho ya Kitaifa ya Nanenane, yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.


Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho (kulia) akifafanua
jambo kwa watumishi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), wakati
alipowatembelea katika maonesho ya Kitaifa ya Nanenane, yanayofanyika katika
viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.


Katibu Mkuu-Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho (kulia) akiangalia baadhi ya Vipuri vinavyochongwa katika karakana ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), wakati alipowatembelea katika maonesho ya Kitaifa ya Nanenane, yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu. Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo upande wa Tanzania, Regina Tarimo.


Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini, Mbaraka Semwanza, akifafanua jambo kwa watumishi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakati alipowatembelea katika maonesho ya Kitaifa ya Nanenane, yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.


Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilangani, akifanunua jambo kwa Afisa
Uhusiano wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Monica Muthoni, wakati
alipowatembelea katika maonesho ya Kitaifa ya Nanenane, yanayofanyika katika
viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akiangalia mashine maalum ya kutotoleavifaranga katika banda la Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), alipotembelea banda hilo Mkoani, katika maonesho ya Kitaifa ya Nanenane, yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akiwa katika picha ya Pamoja na
Watumishi wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam, alipotembelea banda lao katika
maonesho ya Kitaifa ya Nanenane, yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.


Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akizungumza na wafanyakazi wa
Kampuni ya Simu Tanzania, alipotembelea banda hilo katika maonesho ya Kitaifa ya Nanenane, yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu