Home Mchanganyiko MSEMAJI WA FAMILIA:MZEE MKAPA AMEFARIKI KWA MSHTUKO WA MOYO

MSEMAJI WA FAMILIA:MZEE MKAPA AMEFARIKI KWA MSHTUKO WA MOYO

0
Msemaji wa Familia ya Mkapa,Bw.William Urio amesema wanatoa shukrani kwa Serikali ambavyo imekuwa pamoja nao na kushughulikia Msiba huu na wanavyoendelea kushughulikia,wanashukuru kwa uamuzi wa kuanza shughuli za kuaga kwa Misa Takatifu,tunawashukuru Maaskofu kwa kukubali kuendesha Misa.
”Mzee Mkapa alikuwa hajisikii vizuri akaenda Hospitali akaonekana alikuwa na Malaria akaanza matibabu akalazwa Jumatano,Alhamisi mchana aliendelea vizuri nilikuwa nae hadi saa mbili alikuwa anaangalia Live ya chaguzi za wagombea Ubunge Viti Maalum CCM”Msemaji wa Familia ya Mkapa,Bw.William Urio
Aidha Msemaji wa Familia ya Mkapa,Bw.William Urio,amesema kuwa Mzee Mkapa siku ya Alhamisi usiku baada ya kutazama LIVE ya chaguzi Viti Maalum akasikiliza taarifa ya habari, baadaye aliinuka akitaka kutoka akakaa akainamisha kichwa, walipokuja kumpima wakathibitisha kuwa amefariki, sababu ya kifo cha Mzee Mkapa ni mshtuko wa moyo.
#RIPMzeeMkapa