Home Mchanganyiko KAWAWA AAMURU MTENDAJI KATA YA MAKURUNGE KUSWEKWA NDANI

KAWAWA AAMURU MTENDAJI KATA YA MAKURUNGE KUSWEKWA NDANI

0

************************************

NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO
Julai 11
MKUU wa wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Zainab Kawawa, amemuweka ndani Ofisa Mtendaji wa Kata ya Makurunge ,Floliana Kaliamwe, kutokana na matumizi mabaya ya fedha za Serikali.
Kawawa alichukua hatua hiyo baada ya kutoridhishwa na taarifa ya matumizi ya shilingi milioni kumi za Halmashauri, zilizolenga kupauwa vyumba viwili na ofisi shule ya awali Kitongoji cha Mkwajuni, huku Mbunge aliyemaliza muda Dkt. Shukuru Kawambwa akitoa milioni moja ya kuweka kifusi.
Wananchi walilalamikia kukwama ujenzi huo tangu 2018, na kusema ujenzi huo asilimia kubwa umetumika kwa nguvu zao.
Alimhoji Floliana ambaye alisema walipokea milioni 10 mwaka 2018 kwa ajili ya upauaji huo, sanjali na milioni moja iliyotokewa na Dkt. Kawambwa kwa ajili ya kifusi, ambapo Mkuu huyo hakuridhika na taarifa yake ndipo akaamuru Polisi wamchukue.
“Sijaridhika kabisa na taatifa ya matumizi ya fedha za serikali, ambazo ni kodi ya wananchi, pia kigezo kipi kilichotumika kuletwa pesa hizo pasipokuwepo kwa utaratibu wa matumizi ya fedha hizo?,” alihoji Kawawa huku akimuamuru Mkuu wa Polisi amchukue Mtendaji.
Aidha Mkuu huyo amekerwa na Ofisa anayesimamia majengo katika Halmashauri kwa kitendo chake cha kutofika eneo la miradi, hali inayoweza kuchangia kutotekelezwa ipasavyo kazi zinazolenga kuondoa kero za wananchi kwa ufasaha kulingana fedha zinazotolewa.
“Wataalamu kipindi hiki sio cha kukaa maofisini, mnatakiwa kutembelea miradi ambayo inapelekewa pesa za kodi zinazolipwa na wananchi, sipo tayari kuona juhudi za rais wetu John Magufuli zikokwamishwa na watu wachache,” alisema Kawawa mpaka kufikia kuto
Kawawa aliagiza kupatikana kwa taatifa sahihi za matumizi ya fedha hizo ili ajiridhishe, huku alitoa onyo kali kwa watumishi wa Serikali wa ngazi mbalimbali kutekeleza majukumu hao kwa weredi mkubwa, kwani hatokuwa tayari kuona uzembe katika utekelezaji huo.
Mmoja wa wasimamizi wa ujenzi huo alisema kuwa wao walitekeleza majumumu yao ya kusimamia ujenzi huo, kwa kuanza kuweka mbao za kenchi kisha kupiga bati katika vyumba hivyo vitatu vya shule hiyo, kwa lengo la kuwawezesha watoto kuanza elimu ya awali.