Home Siasa Wanyama atiania ya kugombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA

Wanyama atiania ya kugombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA

0

*********************************

Na Magreth Mbinga

Leonard Toja Manyama ametia nia na amechukua fomu ya mgombe wa Urais katika Chama chake cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA .

Yamefanyika hayo leo makoa Makuu ya Chama hiko Kinondoni Jijini Dar es Salaam .

Manyama amesema ameomba kuteuliwa kwasababu anamaono ya kulivusha Taifa ndani ya siku 100 ili kutimiza azma hiyo muhimu atatengeneza mipango ya aina tatu.

Pia amesema anataka kujenga Taifa lenye umoja,upendo, mshikamano na kuondoa chuki za kisiasa na kuondoa hali ya hofu ya kutekwa.

Vilevile Manyama amesema atajikita kurasimisha maeneo ya wananchi wa kipato Cha chini ili kuyaongezea thamani na kuwawezesha kupata mikopo kutoka taasisi za kibenki pamoja na kuondosha kabisa vifurushi vya bima ya afya ili Watanzania wasibaguliwe katika kupewa matibabu.

Sanjari na hayo amesema anamipango ya muda mfupi ambayo watatekeleza ndani ya miaka mitatu mpaka mitano.

Hatahivyo Manyama amesema atakuwa na mipango ya muda mrefu pia ambayo watapanga mikakati ya kuitengeneza Tanzania waitakayo na sio aitakayo mtu fulani.

“Tutaboresha pia mfumo wa utawala ikiwa ni pamoja na kuitenga nchi yetu kuwa katika mikakati maalum ya maendeleo mfano kuainisha miji maalum ya biashara,utalii,viwanda,uvuvi na mambo mengine”amesema Manyama.