******************************
NJOMBE
Shule ya msingi Kitewele iliyopo katika mwambao mwa ziwa Nyasa wilayani Ludewa mkoani Njombe imeendelea kukabiliwa na changamoto kubwa ya miundombinu ya elimu na kusababisha wanafunzi kutohudhuria vipindi na utoro uliokithiri na kupelekea shule hiyo kuathirika kitaaluma kwa kiasi kikubwa.
Shule ya Kitewele iliyopo kata ya Mawengi inakabiliwa na adha kubwa ya upungufu wa madarasa,Maktaba,walimu pamoja na nyumba za kuishi watumishi jambo ambalo limesababisha watoto wengi kutopenda kwenda shule na kuamua kujikita katika uvuvi,kilimo na ufugaji.
Wakizungumzia changamoto zinazokwamisha maendeleo ya taaluma katika shule hiyo January Ngailo ambaye ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kitewele anasema katika shule hiyo kuna changamoto kubwa ya nyumba za walimu ,madarasa na madirisha jambo ambalo limekuwa likisababisha utoaji na upokeaji wa elimu kuwa mgumu.
Wamesema kuna wenzao wanashindwa kufika shule kulingana na kusafiri umbali mrefu kufata elimu jambo ambalo linawafanya kuacha shule na kwenda ziwani kwa uvuvi.
Temba amesema tangu kuanzishwa kwa mradi huo kumekuwa na matokeo chanya katika sekta ya elimu kwani kupitia mradi shule zijengewa madarasa,vyoo ,miradi ya maji sambamba na kupatiwa miradi ya miche ya parachichi .
Zaidi ya shule 20 ikiwemo Kitewele zimejengewa miundombinu ya maji ili kukabiliana na corona.