Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi (katikati) akiwasili katika Viwanja vya Mwl.Julius Nyerere Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam kutembelea Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Wengine ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) Bi.Latifa Khamis na Afisa Habari kutoka tantrade Bi.theresa Chilambo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi (kulia), akimsikiliza Afisa kutoka Bodi ya Sukari Nchini(TSB), alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl.Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi (kushoto), akimsikiliza Afisa kutoka Taasisi ya Soko la Bidhaa Tanzania(TMX) alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl.Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi (kushoto), akimsikiliza mjasiriamali wa zao la korosho ambaye anamuonyesha mashine ya kubangua zao hilo alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl.Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi (mwenye miwani) akifurahia jambo na mashabiki wa Yanga alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl.Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi (kushoto), akiangalia bidhaa itokanayo na zao la pareto alipotembeelea banda la Bodi ya Pareto Nchini (TPB) katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl.Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi(wa tatu kulia) akizungumza jambo na Msanii wa filamu nchini Yvonne Charrie(Monalisa) alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl.Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akiwa katika picha ya pamoja na Wasanii alipotembelea banda lao katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl.Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, akiangalia moja ya tuzo ya Filamu (Bongo Movie), kutoka kwa Gabo Zigamba alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl.Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Picha na Idara ya Habari-MAELEZO
********************************
Na Mwandishi Wetu-MAELEZO
Serikali inaendelea kuziimarisha Bodi za Mazao nchini ili ziweze kutoa huduma bora kwa wananchi kwenye kutafuta masoko na kuwezesha kuuza bidhaa hizo katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
Akizungumza katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi alisema kuwa Serikali imefanya mabadiliko makubwa na sasa bodi za mazao zinafanya kazi sawasawa na dira ya Rais John Magufuli.
“Kwenye hizi bodi Serikali inaendelea kufanya mabadiliko na kuziimarisha ili ziendelee kutoa mchango wake kwenye uboreshaji mazao na masoko kwa wakulima na hasa maeneo mbalimbali ambapo wakulima wanalima mazao ya kimkakati”, Alisema Dkt.Hassan Abbasi
Dkt.Abbasi alisema kuwa bodi za mazao kwa sasa zimejikita katika kuchagiza uzalishaji wa bidhaa na kutafuta masoko zikisaidiana na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Nchini (TanTrade), kwa hiyo Bodi ya Pareto, Chai, Korosho, Pamba, Mkonge, Tumbaku na Sukari zinawasaidia wananchi kutatua changamoto ya masoko.
Alibainisha kuwa kwa sasa bodi za mazao ni mkombozi mkubwa kwa wananchi kwani zinafanya kazi ya kutafuta na kuleta fursa kwenye ngazi zote yaani kilimo na uzalishaji wa bidhaa na hiyo ndiyo dhima kuu ya Serikali kufikia katika uchumi wa kati wenye viwanda ambapo Julai Moja Tanzania ilitangazwa kuingia katika uchumi huo kwa hiyo bodi hizo zinafuata mwelekeo wa Rais John Pombe magufuli.
“Kwenye zile Bodi nimetembelea na kupokea maelezo mengi na ninashukuru kuona kuwa bodi hizi zinaenda mwelekeo ambao Rais Magufuli anautaka, kwani bodi nyingi sasa zinatafuta masoko nje na ndani ya nchi, lakini vilevile zimekuwa mstari wa mbele kwenye uboreshaji wa mazao yetu”, Alisema Dkt.Abbasi.