Home Mchanganyiko NAIBU WAZIRI WA AFYA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA CCBRT

NAIBU WAZIRI WA AFYA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA CCBRT

0

…………………………………………………………………………..

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Godwin Mollel leo Julai 2 alifanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya CCBRT iliyoko Msasani jijini Dar es Salaam

Dk. Mollel alifanya ziara hiyo isiyokuwa rasmi kwa lengo la kuona kazi nashughuli na huduma zinazofanywa katika hospitali hiyo na kuwashukuru wafanyakazi wa Hospitali hiyo pamoja na viongozi kiujumla kwa huduma wanazozitoa kwa jamii.

“Nawafahamu CCBRT na kazi mnazozifanya kwa muda mrefu sasa, nawapongeza kwa kazi nzuri, kama Serikali tunatambua mchango wa hospitali hii katika kuwahudumia watanzania, leo nimefika kusalimia kidogo lakini naahidi kuja rasmi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja ili tuweze kupata wasaa wa kujadilina kwa kina juu ya kazi zenu”. Amesema Dk. Mollel.