Home Mchanganyiko SERIKALI KUBORESHA MAZINGIRA YA UKUSANYAJI TAKWIMU

SERIKALI KUBORESHA MAZINGIRA YA UKUSANYAJI TAKWIMU

0

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango  (Mb), akiweka jiwe la msingi katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mkoa wa Kigoma, kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Rashid Mchata.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (katikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Amina Msengwa, wakipokea hati ya kiwanja eneo ambalo Ofisi ya NBS Mkoa wa Kigoma kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Bw. Rashid Mchata, wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika ofisi hizo mkoani Kigoma.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akimkabidhi hati ya kiwanja  Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Amina Msengwa wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi kwenye jengo la NBS mkoa wa Kigoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia), akipata maelezo ya kazi zinazofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu pamoja na mradi wa ujenzi wa Ofisi za Takwimu za Taifa mkoa wa Kigoma, kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mfumo wa Mawasiliano, Ukusanyaji na Usambazaji wa Taarifa za Kijiografia (GIS), Bw. Benedict Mugambi.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akicheza ngoma na Kikundi maarufu cha Ngoma za asili cha Mapigo Saba cha Ujiji mkoani Kigoma, alipoweka Jiwe la Msingi la Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), mkoani Kigoma.

 

Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa, akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), mkoani Kigoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (walio keti katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kigoma, waliohudhuria hafla ya uwekeji jiwe la msingi la Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mkoa wa Kigoma. Kutoka kushoto ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Ablina Chuwa, Mwenyekiti wa Bodi ya NBS – Dkt. Amina Msengwa, kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya Kigoma, Bw. Samson Anga na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Bw. Rashid Mchata.

               (Picha na Josephine Majura WFM – KIGOMA)

…………………………………………………………………..

Na. Josephine Majura na Peter Haule, WFM, Kigoma

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kazi na mifumo ya ukusanyaji wa takwimu ili kuwa na takwimu bora kwa ajili ya kutunga sera na kupanga mipango endelevu ya maendeleo ya Wananchi ikiwa ni pamoja na kuifanyia tathmini na ufuatiliaji mipango hiyo.

Dkt. Mpango ameyasema hayo wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la Ofisi ya Taifa ya Takwimu Mkoa wa Kigoma ambalo hadi wakati linawekewa jiwe la msingi limegharimu shilingi milioni 173.

“Jengo hili litakapokamilika litaboresha zaidi utendaji kazi kwa watumishi pamoja  na upatikanaji na usambazaji wa takwimu  kwa wadau mbalimbali wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu na hususan wakati  huu wa maandalizi ya zoezi la kitaifa la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika mwaka 2022” alisema Dkt. Mpango

Dkt. Mpango aliipongeza Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa namna ambavyo imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa weledi na kuipatia nchi takwimu bora  ambazo ndizo zinatumika katika kusukuma gurudumu la maendeleo.

“Mafanikio ya Serikali yetu ya Awamu ya Tano ambayo tunajivunia leo yamejengwa kwa msingi mzuri wa matumizi bora ya takwimu ambazo zinazalishwa na taasisi yetu hii’ aliongeza Dkt. Mpango

Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa alisema kuwa ujenzi wa Jengo hilo ni miongoni mwa mikakati ya Ofisi yake ya kuboresha miundombinu itakayo wezesha  matumizi ya teknoljia ya kisasa katika shughuli za ukusanyaji na uchakataji wa takwimu mbalimbali hatua iliyolenga kupunguza matumizi ya Serikali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa  Bodi ya aliishukuru Serikali kwa kutenga fedha za kumalizia jengo hilo na kuomba fedha zilizotengwa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Ofisi hizo zitolewe mapema kwenye robo ya kwanza ya utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2020/21 ili liweze kukamilika mwezi Septemba kama ilivyopangwa.

Ujenzi wa jengo hili ulioanza mwaka 1994 wakati wa Serikali ya Awamu ya Pili chini ya ufadhili wa Ofisi ya Takwimu ya Sweden (Statistics Sweden) iliyokuwa na ushirikiano na Idara Kuu ya Takwimu chini ya Wizara ya Mipango.

Statistics Sweden kwa mujibu wa kumbukumbu zilizoko waligharamia jengo hili kwa jumla ya Shillingi milioni tano mwaka 1994 na Serikali za Awamu ya Tatu, na Nne ziliendelea na juhudi za kugharamia ujenzi wake hadi lilipofikia kwa gharama ya shilingi 173,386,000.