Home Mchanganyiko TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA

0

…………………………………………………………………

TAARIFA YA AJALI YA MTUBWI WA ABIRIA KUPIGWA NA RADI NA KUSABABISHA VIFO NA MAJERUHI KATIKA ZIWA VICTORIA WILAYANI UKEREWE NA MTOTO WA
CHEKECHEA KUSABABISHIWA KIFO NA FISI BAADA YA KUSHAMBULIWA WILAYANI KWIMBA.

TUKIO LA KWANZA
TAREHE 23.06.2020 MAJIRA YA 08:45HRS HUKO KITONGOJI CHA BUSELE, KATA YA BUBIKO WILAYA YA UKEREWE, MTUMBWI WA ABIRIA UNAOJULIKANA KAMA ONE TEN
WENYE NAMBA ZA USAJILI 00238 UNAOFANYA SAFARI ZAKE KATIKA MAENEO YA KOME NA BUGAZA ULIPIGWA RADI, KUSABABISHA VIFO VYA WATU WANNE NA MAJERUHI KWA ABIRIA 27 KATI YAO WANAWAKE 12 NA WANAUME 15 WALIOKUWA WAKISAFIRI.
MAJINA YA WALIOFARIKI NI:-

1. DEOGRATUS MULUNGU, MIAKA 50, MKARA.
2. KUMUNYA ANDREA, MIAKA 36, MKEREWE, MKRISTO,
AMBAYE ALIKUWA NI NAHODHA WA MTUMBWI.
3. SIMON CHERLES, MIAKA 36, MSUKUMA, MKRISTO,
ALIYEKUWA NAHODHA MSAIDIZI.
4. NDEGE ABDU, MIAKA 25, MJITA, KIBARA.
MAJERUHI WAMEFIKISHWA KATIKA ZAHANATI YA KIJIJI
CHA BUKIKO NA WENGINE KATIKA KITUO CHA AFYA
BWISYA KWA AJILI YA MATIBABU NA MIILI YA MAREHEMU
WOTE IMEFANYIWA UCHUNGUZI WA DAKTARI NA
KUKABIDHIWA NDUGU KWA AJILI YA TARATIBU ZA
MAZISHI. MAJERUHI WENGI WAMETIBIWA NA
KURUHUSIWA.

TUKIO LA PILI
TAREHE 22.06.2020 MAJIRA YA 19:00HRS KATIKA KIJIJI CHA MWAMPURU, KATA YA MWANTARE WILAYA YA KWIMBA MTOTO ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA DALAILE
MILAMBO, MIAKA 6, MSUKUMA, MWANAFUNZI WA CHEKECHEA YA MWAMPURU ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUSHAMBULIWA NA FISI SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE WAKATI ALIPOKUWA NA DADA YAKE. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI NA UMEKABIDHIWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA
TARATIBU ZA MAZISHI.

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA KUSHIRIKIANA NA IDARA YA WANYAMPORI NA WANANHI WANAMSAKA FISI HUYO ILI ADHIBITIWE KWA MUJIBU WA SHERIA NA
KUHAKIKISHA KUWA HALETI MADHARA ZAIDI

IMETOLEWA NA:-
Muliro J. MULIRO – ACP
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA