Home Mchanganyiko WIZARA YA KILIMO YASAINI MKATABA WA UJENZI WA KITUO MAHIRI CHA USIMAMIZI...

WIZARA YA KILIMO YASAINI MKATABA WA UJENZI WA KITUO MAHIRI CHA USIMAMIZI WA MAZAO YA NAFAKA

0

Mratibu wa Mradi wa Sumukuvu Bw.Clepin Mbekomize akimpa taarifa kuhusu ujenzi wa kituo Mahiri cha usimamiza wa Mazao ya Nafaka kitakachojengwaa  Mtanana B wilaya ya Kongwa jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya,akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Chakula Dkt.Honest Kessy  kuhusu ujenzi wa kituo Mahiri cha usimamiza wa Mazao ya Nafaka kitakachojengwaa  Mtanana B wilaya ya Kongwa jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya,akizungumza kabla ya kuingia mkataba wa wizara ya kilimo na Kampuni ya M/S BJ AMULI ARCHITECT ambayo ilishinda zabuni ya kufanya ubunifu katika eneo la ujenzi  wa kituo Mahiri cha usimamiza wa Mazao ya Nafaka kitakachojengwaa  Mtanana B wilaya ya Kongwa jijini Dodoma.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya,akiwa pamoja na Mshauri elekezi wa kampuni ya BJ AMULI ARCHITECT  Bw.Nathanieli  Alute wakisaini Mkataba wa Wizara ya kilimo na Kampuni ya M/S BJ AMULI ARCHITECT ambayo imeshinda zabuni ya kufanya ubunifu katika eneo la ujenzi  wa kituo Mahiri cha usimamiza wa Mazao ya Nafaka kitakachojengwaa  Mtanana B wilaya ya Kongwa jijini Dodoma.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya,akiwa  na Mshauri elekezi wa kampuni ya BJ AMULI ARCHITECT  Bw.Nathanieli   Alute wakibadilishana Mkataba baada ya kusaini kati ya  Wizara ya kilimo na Kampuni ya M/S BJ AMULI ARCHITECT ambayo imeshinda zabuni ya kufanya ubunifu katika eneo la ujenzi  wa kituo Mahiri cha usimamiza wa Mazao ya Nafaka kitakachojengwaa  Mtanana B wilaya ya Kongwa jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya,akiwa  na Mshauri elekezi wa kampuni ya BJ AMULI ARCHITECT  Bw.Nathanieli  Alute wakionyesha mkataba mara baada ya kusaini baina ya  Wizara ya kilimo na Kampuni ya M/S BJ AMULI ARCHITECT ambayo imeshinda zabuni ya kufanya ubunifu katika eneo la ujenzi  wa kituo Mahiri cha usimamiza wa Mazao ya Nafaka kitakachojengwaa  Mtanana B wilaya ya Kongwa jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya,akiwa  na Mshauri elekezi wa kampuni ya BJ AMULI ARCHITECT  Bw.Nathanieli  Alute wakipongezana baada ya kusaini Mkataba  baina ya  Wizara ya kilimo na Kampuni ya M/S BJ AMULI ARCHITECT ambayo imeshinda zabuni ya kufanya ubunifu katika eneo la ujenzi  wa kituo Mahiri cha usimamiza wa Mazao ya Nafaka kitakachojengwaa  Mtanana B wilaya ya Kongwa jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya,akitoa maelezo kwa Mshauri elekezi wa kampuni ya BJ AMULI ARCHITECT  Bw.Nathanieli  Alute kuhusu  ujenzi  wa kituo Mahiri cha usimamiza wa Mazao ya Nafaka kitakachojengwaa  Mtanana B wilaya ya Kongwa jijini Dodoma.

Mshauri elekezi wa kampuni ya BJ AMULI ARCHITECT  Bw.Nathanieli  Alute akitoa shukrani kwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya mara baada ya kusaini Mktaba baina ya  Wizara ya kilimo na Kampuni ya M/S BJ AMULI ARCHITECT ambayo imeshinda zabuni ya kufanya ubunifu katika eneo la ujenzi  wa kituo Mahiri cha usimamiza wa Mazao ya Nafaka kitakachojengwaa  Mtanana B wilaya ya Kongwa jijini Dodoma.

 

Sehemu ya wadau wakifatilia matiliano ya mkataba baina ya   Wizara ya kilimo na Kampuni ya M/S BJ AMULI ARCHITECT ambayo imeshinda zabuni ya kufanya ubunifu katika eneo la ujenzi  wa kituo Mahiri cha usimamiza wa Mazao ya Nafaka kitakachojengwaa  Mtanana B wilaya ya Kongwa jijini Dodoma.

…………………………………………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

Katibu Mkuu wa Kilimo Bw. Gerald Kusaya  amesaini mkataba wa ujenzi wa kituo mahiri cha usimamizi wa mazao ya nafaka na Kampuni ya M/S BJ AMULI ARCHITECT ambayo imeshinda zabuni ya kufanya ubunifu katika eneo la ujenzi ambao umegharimu  kiasi cha shilingi billion 16 hadi kukamilika kwa ujenzi wa kituo.

Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dodoma na Wizara ya Kilimo na kampuni ya BJ AMULI ARCHITECT .

Kusaya amesema kuwa mradi wa TANIPAC unatekelezwa katika mikoa 10 ndani ya halmashauri 18 Tanzania Bara na serikali inategemea kujenga maghala 14 katika kituo hicho kitakachojengwa Mtanana B katika halmashauri ya Kongwa jijini Dodoma.

“Tunalenga zaidi usalama wa chakula na ni mapenzi ya Rais ndio maana ametoa hizi pesa kupambana na sumukuvu” amesema Kusaya

Hata hivyo Kusaya amesema kuwa eneo hilo la hekari 150 kitajengwa Kituo mahiri cha usimamizi wa mazao ya nafaka na vihenge ambapo kituo hicho kitakuwa ni cha mafunzo ya kupambana na sumukuvu.

Aidha  Kusaya amemtaka mshauri elekezi wa kampuni hiyo Bw. Nathanieli  Alute kumaliza kazi kwa wakati ili kuepuka kuongezeka kwa gharama kwani kazi yake kubwa ni kufanya ubunifu wa ujenzi wa kituo na anatumaini kuwa kazi itakuwa nzuri kwani kituo kikubwa.

“Nahitaji kuona unafanya hii kazi kwa umahiri na kufanya ubunifu,ufanye kwa wakati na kazi bora,ufanye ndani ya wakati ili isiongezeke gharama ya ujenzi “ amesisitiza Kusaya

Hata hivyo Kusaya ameeleza kuwa wananchi wa mtanana ‘B’ wametoa  ardhi yao bila fidia na nia yao kubwa ni kuona mradi unaenda na wanahitaji kituo ili waweze kupata mafunzo ya namna ya kutunza mazao yao vizuri.

Kwa upande wake Mshauri elekezi wa kampuni ya BJ AMULI ARCHITECT  Bw.Nathanieli Alute ameshukuru kwa kupata fursa hiyo na kuomba ushirikiano na Wizara ili kazi iende vizuri na kukamilika kwa wakati kwani muda waliopewa ni wa miezi mine kwa mujibu wa mkataba.

Hata hivyo amesema watajitahidi  kufanya kazi kama inavyohitajika pamoja na kufanya ubunifu wa majengo yanayohitajika kulingana na ramani ya kituo watakayopewa. Ubunifu huo wa majengo utaanza rasmi kuanzia tarehe 26/06/2020 hadi tarehe 26/10/2020 ndipo atakapotakiwa kukabidhi kazi hiyo.