Home Mchanganyiko SERIKALI YAWATAKA WAZAZI KUSIMAMIA KIKAMILIFU MATUMIZI YA VIFAA VYA KIELEKTRONIKI KWA WATOTO

SERIKALI YAWATAKA WAZAZI KUSIMAMIA KIKAMILIFU MATUMIZI YA VIFAA VYA KIELEKTRONIKI KWA WATOTO

0

 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Mtoto Sebastian Kitiku akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu 

…………………………………………………………………………………..

Na Alex Sonna,Dodoma

Serikali imewataka wazazi au walezi kuwasimamia watoto katika matumizi ya vifaa vya Kielektroniki  ili kuwaepusha kujiingiza katika vitendo vya ngono na ukatili mwingine mitandaoni.

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishiwa Juni 16 kila mwaka.

Mhe.Ummy amesema  kuwa katika kipindi hiki tumeshuhudia watoto wanatumia vifaa ya kielektroniki ikiwa pamoja na simu na komputa kujifunzia, ni vyema watoto wazingatie matumizi sahihi ya vifaa hivyo ili kuepusha kufanyiwa vitendo vya kikatili.

Amesisitiza kuwa Wazazi au Walezi hakikisheni watoto Usalama wa watoto ni muhimu wakati wote na hivyo, watoto wakiwa nyumbani katika kipindi hiki wajiepushe kwenda kwenye maeneo yatakayo hatarisha usalama wao, ikiwa pamoja na kubakwa, kulawitiwa, kushawishiwa kufanya ngono na hata kupata maambukizi ya Corona.

“Katika eneo la malezi ya watoto wetu bado kuna changamoto kubwa ya matumizi ya mitandao tuhakikishe tunawasimamia waotto wetu wasijiingize katika masuala yasiyofaa katika mitandao hiyo” alisema.

Aidha Waziri Ummy amasema kumekuwa na ongezeko la matukio ya vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini ikiwa ni kwasababu wananchi wengi wamepata uelewa na kuweza kutoa taarifa katika maeneo maalum yaliyotolewa na Serikali kutoa taarifa hizo.

Hata hivyo ameitaja  Mikoa ya kipolisi iliyoongoza kuwa na matukio mengi zaidi ya ukatili dhidi ya watoto kwa mwaka 2018 kwa ni Mkoa wa Tanga (1,039), Mbeya (1,001), Mwanza (809) na Arusha (792) na kwa mwaka 2019 ni Mkoa wa Tanga (matukio 1,156), Mkoa wa Kipolisi-Temeke (844), Mbeya (791) na Mwanza (758).

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Mtoto Sebastian Kitiku amesisitiza wazazi kuwajibika kwa kuhakikisha wanawasimamia watoto wako kwa kuhakikisha wanawasimamia na kufuatilia masuala ambayo yanaweza kusababisha ukatili kwa watoto.

“Wazazi tuwaangalie watoto wetu tusiwaache watoto wakajiamulia baadhi ya vitu ambavyo vitawasababisha waingie katika mambo ambayo yatapelekea kufanyiwa vitendo vya kikatili” alisema.

Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika kwa mwaka 2020 inaoongozswa na Kauli mbiu isemayo “Mifumo Rafiki ya Upatikanaji Haki ya Mtoto: Msingi Imara wa Kulinda Haki Zao”