Picha ya Pamoja
mara baada ya makabidhiano hayo leo jijini Arusha kwenye Hafla
iliyofanyika kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha Arusha. Watanzania wameaswa kuendelea kuchukuwa hatua dhidi ya
maambukizi ya Ugonjwa wa homa kali ya mapafu(covid 19) kwa kuendelea
kufuata maelekezo ya wataalam wa Afya nchini kwa lengo la kupambana na
maambukizi mapya. Kauli hiyo imetolewa na kaimu katibu tawala mkoa wa Arusha David
Lyamongi kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa vya kujikinga na
maambukizi ya ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya Corona
kutoka kwa Tahosa mkoa wa Arusha jijini hapa Alisema kuwa serikali ya mkoa inaendelea kuwataka wadau wa
maendeleo kuendelea kushirikiana nayo kuhakikisha wanaendeleza juhudi
za kuutokomeza ugonjwa huo nchini hivyo msaada huo utaendeleza
mapambano ya kukabiliana nao. Akawataka waalimu kuendelea kushirikiana na serikali katika
kuongeza juhudi za kuondokana na changamoto ya Maradhi hayo kwa
kuendelea kuwa mabalozi wa kuhamasisha mapambano ya ugonjwa
huo. “Niwasihi sana waalimu toeni elimu ya usafi kwa jamii yetu
inayowazunguka kuondoa changamoto za magonjwa ya milipuko kwani Elimu
inafaa sana na itasaidia jamii yetu kuwa na uelewa siku za usoni
kuondokana na maradhi au kujikinga nayo” Awali akiongea kwenye hafla hiyo iliyofanyika kwenye ofisi ya
mkuu wa mkoa wa Arusha Afisa Elimu Taaluma mkoa wa Arusha Joseph
Ngoseki alisema kuwa umoja huo walionyesha waalimu hao uendelezwe ili
kuendelea kushirikiana na serikali kupambana na janga la
corona. Kwa Upande wake Katibu wa umoja wa wakuu wa shule Tahosa mkoa wa
Arusha Mwalim Victor Mbwambo alisema kuwa Ndoo hizo 25 walizokabidhi
leo zimelenga kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid 19 na mkoa
utapanga sehemu watakayoona inafaa. Alisema kuwa msaada huo umelenga kuisadia serikali katika
kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu Covid 19 na waliangalia
vifaa hivyo mfano vitakasa mikono barakoa lakini wakaona ndoo zitakuwa
na msaada mkubwa kwani hata kama hakutakuwa na maambukizi mapya
itasaidia kuwaweka safi ili kuepuka magonjwa. |