Home Mchanganyiko MAHAKAMA WETE YAMREJESHA RUMANDE ALIYEBAKA MTOTO WAKE

MAHAKAMA WETE YAMREJESHA RUMANDE ALIYEBAKA MTOTO WAKE

0

………………………………………………………………………

Na Masanja Mabula , Pemba.

MAHAKAMA ya Mwanzo Wete imemrejesha rumande 43  (jina tunalo)anayetuhumiwa kumbaka mtoto wake mwenye umri wa miaka 12

Mahakama hiyo ilifikiaa uwamuzi huo baada ya hakimu wa mahakama ya Mkoa Kaskazini Pemba ambaye anasikiliza kesi hiyo kuwa nje ya mahakama kikazi.

Kwa mujibu wa sheria , kesi za ubakaji zinasikilizwa katika mahakama ya Mkoa , hivyo hakimu wa mahakama ya Mwanzo Maulid Ali Hamad aliipanga shauri hilo kusikilizwa juni 17 mwaka huu.

Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Maulid Ali Hamad , Mwendesha mashtaka koplo Khamis Mzee aliiambia mahakama kwamba , shauri hilo lipo kwa ajili ya kusikilizwa , lakini hakimu husika hayupo mahakamani.

Hati ya mashtaka inaeleza kwamba , mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Novemba 30 mwaka 2019, ambapo bila ya halali alimuingilia mtoto wake huyo ,huku akijua kwamba ni mtoto wake wa kumzaa jambo ambalo ni kosa kisheria.

Kitendo cha kumuingilia maharimu(mtoto)ni kosa kinyume na kifungu cha 143(1)(4) cha sheria namba 6 ya mwaka 2018 , sheria ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.