********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Klabu ya Yanga leo imepokea kichapo cha mabao 3:0 dhidi ya KMC katika mechi ya kupimana nguvu kujiandaa na mechi za ligi kuu kwenye uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya KMC yaliwekwa kimyani na Sadala Lipangile mnamo Dk.31 huku bao la pili likifungwa na Charles Ilanfya Dk.45 na kuwapeleka kipindi cha pili kifua mbele kwa mabao 2:0.
Goli la tatu lilifungwa na Hasan Kabunda Dk.65 na kufanya ubao kusomeka 3:0.Hadi kipyenga cha mwamuzi kupulizwa kumalizika kwa mechi ubao ulisomeka KMC 3:0 Yanga.