RAIS
Dkt. John Pombe Magufuli ameeleza kufarijika kwake kutokana na changamoto
zilizokuwa zikiihusu benki ya Walimu (Mwalimu Commercial Bank plc) sasa
zimeanza kushughulikiwa.

Rais
ametoa kauli hiyo Ijumaa Juni 5, 2020 wakati akihutubia mkutano mkuu wa
uchaguzi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kwenye uwanja wa Jamhuri jijini
Dodoma.

“Najua
chama hiki kina mali na rasilimali mbalimbali, lakini zote hizo ni mali za wanachama
hivyo basi viongozi hawana budi kuhakikisha mali na rasilimali za wanachama
zinatumika kwa malengo yaliyokusidiwa….Na katika hilo nimefarijika kidogo
kusikia kuwa baadhi ya changamoto nilizozitaja kwenye mkutano wa chama cha walimu
Tanzania mwaka 2017 zenye kuihusu benki ya Walimu zimeanza kushughulikiwa.”
Alisema Rais Magufuli.

Aliwataka
viongozi watakaochaguliwa kwenye mkutano huo wa Dodoma waendelee kutatua
mapungufu mengine yaliyobaki kwenye benki hiyo ili wanachama wake wafaidike
kama ilivyotarajiwa wakati wa kuanzishwa kwake.

Awali
katika risala ya wajumbe wa mkutano huo wa uchaguzi iliyosomwa kwa niaba yao na
Katibu Mkuu wa CWT (aliyemaliza muda wake), Mwalimu Deus Seif alisema tangu
walimu wakutane na Rais mwaka 2017 yapo mambo mengi yamefanyika kuhusiana na
benki hiyo ambapo kwa upande wa uongozi kwa sasa chama kina wakilishwa na
walimu wanne katika bodi ya wakurugenzi.

Aidha
kwa upande wa mikopo zaidi ya asilimia 90 imetolewa kwa walimu wakati asilimia
5.3 imetolwa kwa wafanyakazi wengine wa serikali.

Vile
vile Chama Cha Walimu (CWT) kwa kushirikiana na benki pamoja na PSSSF wataweka
utaratibu kwa walimu wastaafu kupokea mafao yao kupitia benki yao ya Mwalimu
Commercial Bank.

“Chama
Cha Walimu kwa kushirikiana na benki tumefikia muafaka kufungua tawi jingine
Dodoma mwishoni mwa mwaka huu ambapo pia benki inaendelea na teknolojia ya
mifumo ya kidijitali ili kufikia walimu wengi katika mikoa mbalimbali nchini.”
Alisema Bw. Seif.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, akihutubia mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Ijumaa Juni 5, 2020
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) wakiwa wamejawa na furaha wakati wa mkutano huo uliofanyika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 5, 2020
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) (Anayemaliza muda wake) Mwalimu Leah Ulaya wakiwapungia mikono wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa chama hicho wakati Rais akiwasili uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Ijumaa Juni 5, 2020
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Mwalimu, Bw. Richard Makungwa (kulia) akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzania (anayemaliza muda wake), Bw. Deus Seif wakati wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa CWT kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Ijumaa Juni 5, 2020