Home Michezo DIEGO COSTA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIEZI SITA JELA KWA KUKWEPA KODI HISPANIA

DIEGO COSTA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIEZI SITA JELA KWA KUKWEPA KODI HISPANIA

0
MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Diego Costa amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela, amacho hatakitumikia na faini ya jumla ya Pauni 482,000 baada ya kukutwa na hatia ya kukwepa kodi zaidi ya Pauni 900,000 mwaka 2014.
Kwa mujibu wa mahakama, mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 31 hakulipa kodi baada ya uhamisho wake Pauni Milioni 4.4 kwenda Chelsea mwaka 2014 na malipo ya haki za pcha zake, zaidi ya Pauni 900,000.
Sheria ya Hispania inatoa fursa kwa wanaohukumiwa kifungo cha chini ya miaka miwili kulipa faini badala ya kuwekwa gerezani.

Diego Costa akitoka mahakamani leo baada ya kulipa fainai ya Pauni 482,000 kukwepa kifungo cha miezi sita jela PICHA ZAIDI SOMA HAPA

Na Costa alikubali kulipa faini ya Pauni 32,000 baada ya kulipa Pauni 450,000 ili kukwepa kuwekwa jela.
Mamlaka ya Kodi Hispania imekuwa mwiba wanasoka nyoata hivi karibuni, ikiwachukulia hatua hadi akina Lionel Messi na Cristiano Ronaldo na kocha wa zamani wa Real Madrid, Jose Mourinho na hakuna kati yao aliyetumikia kifungo baada ya wote kulipa faini.