Home Mchanganyiko IGP SIRRO AWAONYA WANASIASA

IGP SIRRO AWAONYA WANASIASA

0

*******************************

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewaonya wanasiasa nchini na kuwataka wafanye siasa zao na kutokuingili vyombo vya ulinzi na usalama na kuviacha vitimize wajibu wao uliopo kisheria.

 

IGP Sirro amesema hayo leo akiwa mkoani Simiyu wakati alipofanya ziara ya ukaguzi katika mkoa huo na kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo
ambapo alisema kuwa Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha linasimamia sharia zote ikiwemo za usalama barabarani.

 

Aidha, IGP Sirro amewapandisha vyeo askari wawili wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia FFU mkoa wa Simiyu kutoa cheo cha konstebo wa Polisi na kuwa Koplo wa Polisi kutokana na umahili wao wa kutekeleza majukumu wanayopewa.