Home Mchanganyiko TAARIFA KWA UMMA JUU YA OPERESHENI MAALUM YA KUDHIBITI VITENDO VYA KIUHALIFU...

TAARIFA KWA UMMA JUU YA OPERESHENI MAALUM YA KUDHIBITI VITENDO VYA KIUHALIFU IKIWEMO WIZI WA PIKIPIKI KWA MIKOA YA KANDA YA ZIWA

0

Ndugu waandishi wa habari, hali ya usalama katika mikoa yetu ya Kanda ya Ziwa imeendelea kuwa shwari. Hii imetokana na juhudi kubwa inayofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama pamoja na raia wema. Hata hivyo napenda kutoa taarifa ya Operesheni inayoendelea katika Mikoa yetu hii.

IKUMBUKWE: Tarehe 24/04/2020 Afande Inspekta Jenerali wa Polisi alifanya kikao kazi na Makamanda wa Polisi na Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa, kilichofanyika katika Mji wa Musoma uliopo Mkoa wa Mara. Katika kikao hicho alipata taarifa ya operesheni dhidi ya makosa ya mauaji iliyoshirikisha mikoa sita ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza, Geita, Simiyu, Tabora, Shinyanga na Kagera. Operesheni hiyo ilifanyika kufuatia maelekezo yake ya awali ambayo aliyatoa kwa Makamanda wa Polisi wa mikoa ya Kanda ya ziwa kilichofanyika tarehe 22/01/2020 huko mkoani Shinyanga. 

Afande Inspekta Jenerali wa Polisi alielekeza kufanya operesheni maalumu dhidi ya wimbi la ongezeko la uhalifu wa wizi wa pikipiki katika mikoa ya Kanda ya Ziwa hali ambayo inatishia amani katika maeneo hayo. 

Hivyo kwa mazingira hayo, operesheni hii ilianza rasmi tarehe 04/05/2020 kufuatia kazi iliyofanyika kwa wiki moja ya kukusanya taarifa za kiintelijensia na za kiuhalifu.

Operesheni hii imechukuwa muda wa takribani mwezi mmoja kuanzia tarehe 04/05/2020 hadi tarehe 29/05/2020 na inahusisha mikoa nane ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza, Geita, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Tarime Rorya, Mara na Kagera

MAFANIKIO YALIYOTOKANA NAOPERESHENI

Jedwali lifuatalo linaonyesha mchanganuo wa mafanikio yaliyotokana na Operesheni hii  kwa kipindi cha mwezi mmoja;

S/No KOSA IDADI  YA MALI/SILAHA ZILIZOKAMATWA  IDADI YA KESI IDADI YA WATUHUMIWA WALIOKAMATWA
1 MALI MBALIMBALI ZIDHANIWAZO KUWA ZA WIZI 792 296 296
2 WIZI WA PIKIPIKI 14 14 14
3 KUPATIKANA NA SILAHA 03 03 03
4 MALI ZA KUOKOTA 12
5 KUPATIKANA KWA WATUHUMIWA WA MAUAJI 03 03
6 MAKOSA MENGINE 37 37
7 WIZI WA TAIRI 04 01 01
                                                                                                    JUMLA 825 354 354

Katika Operesheni hii jumla ya mali/pikipiki zilizokamatwa ni 825 na jumla ya kesi zilizofunguliwa ni 354 kama ilivyoainishwa hapo juu.

NAMNA MASHAURI YA OPERESHENI YALIVYOSHUGHULIKIWA KWA KILA MKOA

S/No HATUA TABORA MWANZA SIMIYU SHINYANGA TARIME RORYA MARA GEITA KAGERA JUMLA
1 IDADI YA KESI ZILIZOFUNGULIWA 43 19 36 19 38 09 97 92 353
2 IDADI YA MALI/PIKIPIKI ZILIZOKAMATWA 41 18 79 27 61 98 446 92 862
3 KESI ZILIZOPELEKWA MAHAKAMANI 20 01 08 01 06 17 07 60
4 IDADI YA KESI ZILIZOPATA MAFANIKIO 10 02 12
5 KESI ZILIZOFUNGWA POLISI 11 05 16
6 KESI ZILIZO CHINI YA UPELELEZI 12 05 28 25 43 09 80 85 287
7 PIKIPIKI ZILIZOTOZWA FAINI 76 165 241
8 IDADI YA MAGARI YALIYOKAMATWA 02 02 02 06

  • Mkoa wa Mwanza walikamatwa watuhumiwa 12 na injini za boti 106 katika visiwa vya Juma, Gembale na Zilagula vilivyopo katika wilaya ya Sengelema

  • Katika operesheni hii Mkoa wa Tabora wamekamatwa watuhumiwa halisi watatu wa mauaji

  • Aidha katika kipindi hiki cha Operesheni, Mkoa wa Geita wamekamatwa watuhumiwa wawili wa wizi wa matairi manne ya Gari aina ya Toyota Surf  T 477 ACY. Katika kufanikisha tukio hilo watuhumiwa walitumia bajaji namba MC 688 BXA TVS KING kwenye ubebaji wa tairi hizo nayo pia imekamatwa na inashikiliwa ili taratibu za kisheria ziweze kufuatwa.

YALIYOBAINIKA  KATIKA OPERESHENI HII

  • Kufatia Janga la COVID -19 Askari walichukua tahadhari kubwa katika kufanikisha ukamataji.

  • Wamiliki wengi wa vyombo vya moto hususani pikipiki hawana uelewa wakutosha kuhusu umiliki, utunzaji, kuazima na hata kukodisha kwa mfano mmiliki anamkabidhi mtu pikipiki bila mikataba au kumjua kiundani anayemkodisha au abiria wake.

  • Pikipiki nyingi kuwa na namba za kampuni inayouza hata kama iliuzwa kwa mtu zaidi ya mmoja.

  • Watu wanachonga namba za pikipiki ilihali hawana vibali au leseni za kufanya kazi hizo. Mfano kwa mkoa wa Mara wamekamatwa watuhumiwa watatu wanaohuka na kuchonga namba za pikipiki.

RAI. Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wananchi wote kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu mapema kabla madhara hayajatokea kwani wahalifu wapo kwenye jamii zetu, hivyo jamii inapaswa kuuchukia uhalifu ili nchi yetu iwe na amani.

KWA UMOJA WETU TUNAWEZA KUUTOKOMEZA UHALIFU WA AINA ZOTE

Asanteni kwa kunisikiliza.

Imetolewa na:  MIHAYO K.MSIKHELA – SACP

MKUU WA OPERESHENI MAALUM ZA JESHI LA POLISI