Home Mchanganyiko TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

0

…………………………………………………

Mnamo tarehe 18/5/2020 majira ya saa 03:00 usiku huko katika mtaa wa Ibala Kata ya Uyole Tarafa ya Iyunga karibu na hospitali ya Sijabaje  – Uyole Jiji na Mkoa wa Mbeya, JONAS YOHANA MAHENGE @ MWARABU [52] Mfanyabiashara na Mkazi wa Ibala Uyole alijiua kwa kujipiga risasi mdomoni na kutokea utosini kwa kutumia silaha yake ndogo aina ya Pisto Browning yenye namba A920533 Car namba ya usajili 00099307 kiini cha tukio kinachungunzwa.

Ni kwamba marehemu alikuwa mfanyabiashara ya Mbao, Mabanzi na viazi na pia alijihusisha na uchimbaji madini Chunya.

Hivi karibuni aliomba mkopo katika benki ya CRDB wa Tshs milioni mia moja. Marejesho ya fedha hizo yalimtatiza akaamua kuuza nyumba yake na kupunguza deni hilo.

Baadae benki walimpa sharti la kuwa anarejeshe kila mwezi Tshs  Milioni tatu kitu ambacho alishindwa kutokana na biashara ya madini Chunya alikokuwa anapeleka hela mara kwa mara bila kupata faida.

Usiku wa tarehe 18/05/2020 waliamka familia usiku saa nane kwa ajili ya kujifukiza kutokana na magonjwa mbalimbali; wakati wenzake wameamka na kwenda kwenye maandalizi yeye alirudi na kujifungia ndani akachukua silaha yake na kujipiga risasi mdomoni ikatokea kisogoni/utosini.

WITO WA KAMANDA.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi ULRICH MATEI anatoa pole kwa familia ya MAHENGE na Wafanyabiashara wote wa Mbeya kwa msiba huo mzito wa kumkosa mhimili wa familia na mwenzetu.

Jeshi la Polisi linashauri wananchi na Watanzania kwa ujumla kuwa na mpango mkakati [Strategic plan] wakati wa kufanya shughuli za kiuchumi zozote kabla ya kuchukua mkopo wowote. Pia tunashauri watu wote kabla ya kufanya biashara yoyote tuwashirikishe wataalamu wa biashara kwa ushauri [Business Consultancy] ili washauri mapato na matumizi ya biashara zetu.

Jeshi la Polisi linashauri familia ikiona mmoja wa mwanafamilia anamiliki silaha na amebadilika afya ya akili kutokana na mazingira yoyote yale nashauri watoe taarifa kwa Jeshi la Polisi ili silaha iwekwe kituoni kwa muda ili kuepusha madhara makubwa yasitokee. 

KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].

Mnamo tarehe 15.05.2020 majira ya saa 15:20 Alasiri huko Kijiji cha Bugoba, Kata ya Kisondela, Tarafa ya Pakati, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata TUKUPASYA AUGUSTINO MWAFILOMBE [41] Mkazi wa Bugoba akiwa na pombe haramu ya moshi [gongo] lita 21. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa pombe hiyo.

KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI BILA KIBALI.

Mnamo tarehe 16.05.2020 majira ya saa 16:30 jioni huko Kitongoji cha Kilambo, Kata ya Njisi, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata MARKO KANDONGA [78] Mkazi wa Kilambo akiwa na ngozi moja ya mnyama ya Komba [Bushbaby], ngozi moja ya nyoka Chatu [Python] na mkia wa mnyama ya Ngiri [Warthog]. Thamani ya nyara hizo bado kujulikana. ufuatiliaji unaendelea.

KUPATIKANA NA POMBE YA MOSHI [ GONGO].

Mnamo tarehe 16.05.2020 majira ya saa 13:30 mchana huko Kitongoji cha TulienI, Kijiji cha Mafyeko, Kata ya Mafyeko, Tarafa ya Kipembawe, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi waliwakamata PILI BUNDALA [44] Mkazi wa Tulieni na MWALU LUHENDU [37], Mkazi wa Tulieni wakiwa na pombe haramu ya moshi [gongo] lita 25. Watuhumiwa ni wauzaji na watumiaji wa pombe hiyo.

KUPATIKANA NA BHANGI.

Mnamo tarehe 16.05.2020 majira ya saa 17:00 jioni huko Mtaa wa Makunguru, Kata ya Ruanda, Tarafa ya Sisimba, Jiji la Mbeya. Askari Polisi waliwakamata SHUKURU LUGANO [18], na SHUKURU PETER [21] wote wakazi wa Makunguru wakiwa na bhangi kilo 03. Watuhumiwa ni wauzaji na watumiaji wa bhangi.

KUPATIKANA NA POMBE YA MOSHI [ GONGO].

Mnamo tarehe 17.05.2020 majira ya saa 12:00 Mchana huko Kijiji cha Kikota, Kata ya Kiwira, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi waliwakamata YOHANA KFRANK MBANDE [42] Mkazi wa Lukwego – Kikota akiwa na pombe haramu ya moshi [gongo] lita 4.5 na IZRAEL SIMON KAJAMBA [51] Mkazi wa Lukwego – Kikota akiwa na Pombe haramu ya moshi [gongo] lita 06. Watuhumiwa ni wauzaji na watumiaji wa pombe hiyo.

KUPATIKANA NA BHANGI.

Mnamo tarehe 17.05.2020 majira ya saa 07:30 Asubuhi huko Kitongoji cha Mtakuja, Kijiji cha Majengo, Kata ya Nkung’ungu, Tarafa ya Kipembawe, Wilaya wa Chunya, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata GIFTING PYELI @ MWAKISISILE [32] Mkazi wa Mtakuja – Majengo akiwa na bhangi gramu 240. Mtuhumiwa ni muuzaji na mutumiaji wa bhangi.