Home Mchanganyiko RC MAKONDA ATANGAZA VITA NA WANAOPANDISHA BEI YA SUKARI, MSAKO MKALI KUANZA...

RC MAKONDA ATANGAZA VITA NA WANAOPANDISHA BEI YA SUKARI, MSAKO MKALI KUANZA KESHO.

0

************************************

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametangaza vita na Wafanyabiashara wanaouza Sukari kwa bei ghali tofauti na bei elekezi ya Serikali ambapo amesema ifikapo Kesho kikosi kazi kitafanya ukaguzi na watakaobainika kuuza bidhaa hiyo kwa bei ya juu Watakamatwa na Sukari kutaifishwa na Serikali.
RC Makonda amewaelekeza Wakuu wa Wilaya zote Tano za Mkoa huo kuhakikisha msako huo unaanza kesho na asisalie Mfanyabiashara yoyote anaeuza Sukari hiyo kwa Bei ya Juu.
Hatua hiyo imekuja baada ya RC Makonda kubaini uwepo wa baadhi ya wafanyabiashara wanaouza Sukari kwa bei ya hadi Tsh 4,500 kinyume na bei elekezi ya serikali ya Tsh 2,600 jambo linalopelekea maumivu na gharama kwa wananchi.