Home Burudani SARAH MAGESA AOMBA WATU WA KUMSIMAMIA KATIKA MUZIKI.

SARAH MAGESA AOMBA WATU WA KUMSIMAMIA KATIKA MUZIKI.

0

********************************

MWIMBAJI anayefanya vizuri katika muziki wa Injili Tanzania, Sarah Magesa amejitokeza hadharani kuomba Msaada ya wa menejimenti kwa Muziki wake.

Sarah amesema muziki kwa sasa unahitaji watu wengi wa kukusapoti na sio kusimama pekee yake Kama alivyoanza kuimba kipindi Cha Mwanzo.

“Unajua Muziki wa Sasa una mahitaji mengi Sana ambayo Mwimbaji pekee yake hawezi kuyatimiza, pamoja kuwa anaweza kufanya Mambo mengi Ila Kuna mahala unahitaji watu wengine wakusaidie’ alisema Sarah

“Pamoja na Mungu kukutangulia, pia Mungu huyo huyo huwa ana taratibu ya kukuinulia watu wa kusapoti katika Maeneo mengi Kama kwenye Promosheni, Masoko na mauzo ya bidhaa anazozalisha Mwimbaji”.

“Ni kweli kwa sehemu tunajua Mambo mengi Ila huwezi kujua kila kitu, unahitaji watu wabobevu ambao wanajua Mambo ya muziki wakusaidie kukushauri njia sahihi ya kupita huku Mungu akikuongoza”

Sarah Magesa ni Mwimbaji anayefanya vizuri Sana kwa Sasa na anatamba na wimbo wake wa uitwao “Nimebaki na Wewe” ambao umetazamwa na watu wengi katika mtandao wa Yutubu.