Home Mchanganyiko WAWILI WAFARIKI ARUMERU KUFUATIA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA

WAWILI WAFARIKI ARUMERU KUFUATIA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA

0

****************************************

Watu wawili wamefariki Dunia kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha kwa siku tatu mfululizo katika wilaya ya Arumeru

Akitoa Taarifa za hali ya mwendendo wa mvua hizo mara baada ya kufanya ziara na kushiriki shughuli za uokoaji, Mkuu wa wilaya ya Arumeru amesema mvua zimeleta madhara makubwa kufuatia watu wawili kufariki leo Alhamisi Tarehe 23/04/2020 Katika Halmashauri ya Meru

Dc Muro amewataja waliokufa kuwa ni Ndugu Kifo Terevaeli mirisho nasari Mwenye miaka 65 Mkazi wa kitongoji cha meto kijiji cha mulala kata ya songoro, ambapo amefariki Dunia Asubuhi baada ya maporomoko ya Udongo kutoka mlimani kuvunja ukuta wa chumba alichokuwa amelala na kufariki Dunia papo hapo, na tayari mwili wake umepatikana na kupelekwa katika hospital ya Mount Meru.

Dc Muro pia amesema kifo kingine na ni cha mtoto alietambuliwa kwa majina ya Tumaini Simon Mwenye umri wa miaka 3 Mwenyeji wa kijiji cha Valeska Kitongoji cha Mwamko, ambae amesombwa na mafuriko ya maji wakati akiwa katika harakati za kuokolewa na Mzazi wake ambapo Mzee simon alifanikiwa kuokoa mtoto mmoja na mwingine kufariki dunia na mwili wa mtoto tumaini umepatikana na taratibu za mazishi zinaendelea.

Katika Mvua hizo Dc Muro amesema zaidi ya Nyumba 50 zimeharibiwa uku zingine zikianguka kutokana na maji kuwa mengi na tayari ameshaziagiza kamati za maafa zinazonongozwa na wakurugenzi wa Halmashauri za Meru na Arusha kushirikiana na wananchi katika kutoa misaada ya haraka katika kunusuru familia hizo ikiwemo kuwatafuta makazinya muda, na kutoa tahadhari ya wananchi waliojenga pembeni ya milima na miinuko mikubwa pamoja na wale waliojenga Katika maeneo yanayokumbwa na mafurko kuondoka katika maeneo yao haraka kabla ya madhara zaidi mana mvua bado zinaendelea kunyesha