Home Mchanganyiko RPC TANGA WAONYA WEZI,AWAAMBIA WAKAOKAMATWA WATAWAFINYANGWAFINYANGWA WASAHAU WALIPOTOKEA

RPC TANGA WAONYA WEZI,AWAAMBIA WAKAOKAMATWA WATAWAFINYANGWAFINYANGWA WASAHAU WALIPOTOKEA

0

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Blasius Chatanda akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali

 KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Blasius Chatanda akiwaonyesha waandishi wa habari vitu ambavyo
vimekamatwa wakati wa opeseheni hiyo


Camera ambazo pia zimekatwa wakati wa operesheni hiyo,

**************************************

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Blasius Chatanda ametoa onyo kali kwa wezi wanaovunja nyumba za watu na kuiba mali kwa kuwataka waache mara moja tabia hiyo kabla
hawajawafinyangwa finyangwa.

Chatanda aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kwamba awali kulikuwa kumeibuka wimbi la uvunjaji wa nyumba hali ambayo iliwalazimu kuanzisha operesheni kabambe ya kuwasaka ili kuhakikisha wananchi wanaishi kwa
amani.

Alisema kwamba katika operesheni hiyo walifanikiwa
kuwakamata watuhumiwa 8 ambao kwa sasa wapo mahabusu ambapo walikamatwa wakiwa na vitu mbalimbali ambavyo waliviiba kwenye maeneo mbalimbali
Jijini Tanga.

Kamanda Chatanda alitaja vitu ambavyo vilikamatwa
kuwa ni TV Flat Screen 7zenye ukubwa wa tofauti kuanzia nch 50 hadi 21 ambazo zinadaiwa ziliibiwa kwenye baadhi nyumba za kulala wageni zilizopo Jijini Tanga.

Aidha alisema pia katika operesheni hiyo waliwakamata vitu vingine ikiwemo Kompyuta mpakato 16,simu za mkononi 7 ambapo baadhi ya vitu hivyo viliibiwa kwenye nyumba za kulala wageni.

“Tunaomba walioibiwa waje watambue mali zao
kama ni miongoni mwa zilizokamatwa huku akisisitiza kwamba msako huo ni endelevu na hakuna mtu ambaye hatabaki salama “Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Tanga.

Kamanda huyo alisema kwamba msako huo ni endelevu na
hakuna mtu ambaye atabaki salama huku akieleza kwamba kwa waliozoea kuiba watafute kazi nyengine za kufanya kwa sababu wakikamatwa watawafinyangwafinyanwga mpaka wasahau njia walizokujia.