Home Mchanganyiko KAMPUNI YA G1 SECURITY YAMPATIA RC MAKONDA MCHANGO WA GENERATOR KWAAJILI KUSAIDIA...

KAMPUNI YA G1 SECURITY YAMPATIA RC MAKONDA MCHANGO WA GENERATOR KWAAJILI KUSAIDIA MAPAMBANO DHIDI YA CORONA.

0

************************************

Kampuni ya Ulinzi ya G1 Ltd leo imeunga mkono Juhudi za serikali ya Mkoa wa Dar es salaam katika Mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona kwa kutoa Generator moja kwaajili ya kuzalisha umeme kwenye Vituo vilivyotengwa kwaajili ya tatizo la Corona kama ikitokea dharura ya umeme ukikatika.

Akipokea Mchango huo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda, Mganga mkuu wa Mkoa huo Dr. Rashid Mfaume ameishukuru Kampuni hiyo kwa kuunga mkono juhudi za serikali ambapo ameeleza licha ya kutoa Generator hiyo pia walitoa Ambulance moja ambayo inaendelea kutoa huduma kwenye Hospital ya Mloganzila.

Kwa upande wake Afisa rasilimali watu wa Kampuni ya G1 Security Ltd Bw. Seleman Yusuph amesema Kampuni hiyo itaendelea kushirikiana ofisi ya Mkoa katika masuala mbalimbali ya kijamii.