Home Mchanganyiko BENKI YA TPB YAKABIDHI MSAADA WA MIFUKO 200 YA SARUJI UJENZI WA...

BENKI YA TPB YAKABIDHI MSAADA WA MIFUKO 200 YA SARUJI UJENZI WA MADARASA YA SHULE MKOANI RUKWA

0

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa Reiner Rukalah (katikati) akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa  mifuko 200 ya saruji yenye thamani ya shilingi milioni 3.7 kutoka kwa benki ya TPB. Mifuko hiyo itakwenda kusaidia ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa ya shule mbalimbali Mkoani hapo. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum wa Rukwa Bupe Mwakang’ata na kulia ni Meneja wa benki ya TPB tawi la Sumbawanga Damas Joseph. Hafla hiyo fupi ya makabidhiano ilifanyika kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Rukwa.

Mbunge wa Viti Maalum wa Rukwa Bupe Mwakang’ata akishukuru baada ya kupokea msaada wa mifuko 200 ya saruji yenye thamani ya shilingi 3.7  kutoka benki ya TPB. Mifuko hiyo itakwenda kusaidia ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa ya shule mbalimbali Mkoani hapo. Kulia ni Mkurugenzi wa Teknohama na Uendeshaji wa benki ya TPB Jema Msuya, na kushoto ni Meneja wa benki ya TPB tawi la Sumbawanga Damas Joseph. Hafla hiyo fupi ya makabidhiano ilifanyika kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Rukwa.

Mkurugenzi wa Teknohama na Uendeshaji wa benki ya TPB Jema Msuya (kushoto) akikabidhi mifuko 200 ya saruji yenye thamani ya shilingi 3.7 milioni kwa Mbunge wa CCM  Viti Maalum Mkoa wa Rukwa Bupe Mwakang’ata kwa ajili ya kusaidia ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa ya shule mbalimbali Mkoani hapo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa Reiner Rukalah.

Mkurugenzi wa Teknohama na Uendeshaji wa benki ya TPB Jema Msuya (kushoto) akikabidhi mifuko 200 ya saruji yenye thamani ya shilingi milioni 3.7 kwa Mbunge wa CCM  Viti Maalum Mkoa wa Rukwa Bupe Mwakang’ata kwa ajili ya kusaidia ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa ya shule mbalimbali Mkoani hapo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa Reiner Rukalah na Mwenyekiti wa UWT Mkoa Maria Kalula.