Home Michezo ARSENAL YAFUTA RATIBA YA MAZOEZI

ARSENAL YAFUTA RATIBA YA MAZOEZI

0
………………………………………………………………………………………..
Timu ya Arsenal, imefuta mpango wake wa kuanza mazoezi Jumanne ya wiki hii na imewataka wachezaji wake kuendelea kukaa nyumbani kutokana na hatari ya Virusi vya Corona.
Kikosi cha kwanza cha Arsenal, kilitarajiwa kuanza mazoezi juma hili, kufuatia wachezaji, benchi la ufundi na wafanyakazi wote, kumaliza siku 14 za kujitenga, ambazo walipewa siku chache baada ya kocha mkuu, Mikel Arteta, kubainika kuwa na maambukizi ya Virusi vya Corona .