Home Burudani MSANII WA VICHEKESHO, IDRIS SULTAN KIZIMBANI KWA KOSA LA KUCHAPISHA MAUDHUI MTANDAONI

MSANII WA VICHEKESHO, IDRIS SULTAN KIZIMBANI KWA KOSA LA KUCHAPISHA MAUDHUI MTANDAONI

0
 Msnii wa vichekesho nchini, Idris Sultan akiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
MSANII wa vichekesho nchini, Idris Sultan na wenzake wawili wamefikishwa leo Machi 20,2020 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wakikabiliwa na kosa moja la kuchapisha maudhui mtandaoni bila kibali cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Doctor Ulimwengu na Isihaka Mwinyimvua ambapo wote kwa pamoja walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa makosa yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi na Wakili wa Serikali, Batlida Mushi.
 Wakili Mushi amedai kuwa Idris na wenzake wametendeka kosa hilo kati ya Machi 8, 2016 na Machi 12, 2020 katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam.
Imedaiwa katika maeneo hayo walirusha maudhui kupitia chaneli ya YouTube huku wakiwa hawana kibali cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA.
Baada ya kusomewa mashitaka hayo, washitakiwa wote walikana kutenda kosa hilo ambapo wakaachiwa kwa masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja kwa kila mshitakiwa ambao wamesaini bondi ya Sh.Milioni nane kila mmoja.
Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyi hadi Aprili 21,2020 ambapo itarudi kwa ajili ya kusikilizwa.