Home Siasa ”NI DHAMBI KUTUMIA SHIDA ZA WATU KUTENGENEZA FAIDA KWA HILA”-CCM

”NI DHAMBI KUTUMIA SHIDA ZA WATU KUTENGENEZA FAIDA KWA HILA”-CCM

0

…………………………………………………………………………….

Na Magreth Mbinga

Chama cha mapinduzi CCM kimesema ni dhambi kubwa kutumia shida za watu kutengeneza faida kwa hila.

Hayo yamezungumzwa na katibu mwenezi wa chama hiko Hamphlei Polepole katika mazungumzo yake na waandishi wa habari katika kutoa msimamo wa chama kuhusu ugonjwa wa virusi vya (COVID 19) maarufu kama Corona.

Pia Polepole amesema wao kama chama cha mapinduzi wameelekeza serikali kuweka Hali ya utayali katika maeneo yote ya mipaka ya nchi kuanzia baharini,maziwa,nchi kavu na viwanja vya ndege.

“Chama cha mapinduzi tumepokea taarifa kutoka serikalini kupitia waziri wa afya na Rais katika ziara yake siku ya Jana”amesema Polepole.

Vilivile amesema serikali imesimamisha shughuli za mbio za mwenge ili pesa hiyo isaidie katika harakati za kupambana na virusi hivo vya Corona.

“Shughuli zote zinazo husisha mikusanyiko iwe ya hazara au ya ndani kwenye chama cha mapinduzi imesitishwa kuanzia leo mpaka pale litakapotolewa tamko la kuruhusu mikutano ili kuepusha maambukizi ya ugonjwa huo yasienee kwa kasi”amesema Polepole.

Sanjari na hayo Polepole amesema ziara zote za viongozi wa chama hiko zimesimamishwa kwaajili ya usalama na kinga dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huo.

“Wafanya biashara wote ambao wanahusika na kuuza vimiminika ambavyo vina toa kinga dhidi ya ugonjwa huo wauze kwa bei elekezi ambayo imetolewa na msd na kama havita patikana kwa wingi mtaani maduka ya msd yanatoa vimiminika hivo kwa bei ileile “amesema Polepole.