Home Mchanganyiko TANGA UWASA YAWEKA BAYANA VISABABISHI VYA BILI KUBWA ZA MAJI

TANGA UWASA YAWEKA BAYANA VISABABISHI VYA BILI KUBWA ZA MAJI

0

 Afisa
Uhusiano wa Mamlaka hiyo Devota Mayala kulia akitoa ufafanuzi wa huduma
za mamlaka hiyo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari wakati
alipotembelea banda lao kwenye eneo la viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga
wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa
ilifanyika eneo hilo

 Sehemu
ya watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa mazingira Jijini
Tanga (Tanga Uwasa) wakiwa kwenye maandamano kuelekea kwenye viwanja vya
CCM Mkwakwani mjini Tanga

 Sehemu
ya watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa mazingira Jijini
Tanga (Tanga Uwasa) wakiwa kwenye maandamano kuelekea kwenye viwanja vya
CCM Mkwakwani mjini Tanga

Sehemu
ya watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa mazingira Jijini
Tanga (Tanga Uwasa) wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye banda lao

 
MAMLAKA
ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) imeeleza
kwamba vitu ambavyo vinasababisha bili za maji kuwa kubwa ni matumizi ya
maji na kutokukaguliwa kwa miundombinu iliyopo kwenye nyumba mara kwa
mara kama bomba linavuja au limedondokewa na kitu kupasuka na kumwaga
maji .

Upasukaji huo wakati mwengine umekuwa hautambuliki mapema
na hivyo kupelekea ongezeko la bili kubwa jambo ambalo lingeweza
kudhibitiwa iwapo kungekuwa na utaratibu nzuri wa kufanyika ukaguzi huo
mara kwa mara kwenye miundombinu hiyo.

Hayo yalisemwa leo na
Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Devota Mayala wakati akizungumza na
waandishi wa habari wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
ambapo kimkoa ilifanyika kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga.

Alisema
kwamba walitumia siku hiyo pia kutoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma
zao za maji safi na uondoshaji wa maji taka ambapo katika suala hilo
mtumiaji mkubwa ni mwanamke kwa sababu walipaji wa bili ni wakina baba
na watumiaji wakubwa ni wakina mama ndio wanatumia kwa ajili ya matumizi
mbalimbali.

“Bili kubwa inasababishwa na vitu vingi ikiwemo
matumizi ya maji, miundombinu iliyopo kwenye majumba yetu kama watu
hawana utaratibu wa kukagua mabomba unakuta linamwaga maji au
limedondokewa na kitu likapasuka bila watu kujua na hivyo maji
yakimwagia kwenye mita inaandika maji yametumika”Alisema

Alisema
kitu kingine ni hitilafu kwenye mita hali inayochangia uwepo wa bili
kubwa ambazo huzielewi huku gharama unazolipa zisizo sahihi unaruhusiwa
kufika ofisini na kuonana na wahusika na kuambiwa ufanye nini ili
ikiwemo upimaji wa mita yako.

Hata hivyo alisema mita itapimwa
na utaonyeshwa kama inashida na baadae itabadilishwa kwa hiyo wapo
kwenye maadhimisho hayo kuwaelimisha wakina mama na wananchi kuhusiana
na suala hilo.

Awali akizungumza Afisa Utawala wa Tanga Uwasa
Theresia Sanga alisema kwamba wataendelea kutoa elimu kuhusiana na
uondoshaji maji taka majumbani ikiwemo kuacha kufanya uhujumu wa
miundombinu ya maji na maji taka.

Aliwataka wananchi
waliounganishwa na mtandao wa maji taka kuutumia vizuri na kutokuweka
taka ngumu kwani inaweza kupelekea kutokupitisha maji vizuri.

“Lakini
pia nitoe wito kwa wananchi kwenye maeneo ambayo mtandao wa maji taka
umepita wateja wajiunge na mtanda huo pamoja na kuacha kuhujumu
miundombinu hiyo kwa kutupa taka ngumu kwani wanakuwa wakiihujumu
taasisi hiyo kwani wanatumia fedha nyingi kuirejesha kwenye hali yake ya
kawaida”Alisema