Home Mchanganyiko WANAWAKE WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA   WATOA MKONO WA FARAJA KITUO CHA...

WANAWAKE WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA   WATOA MKONO WA FARAJA KITUO CHA NYUMBA YA MATUMAINI MIYUJI

0

Msimamizi  wa kituo hicho Sista Anitha Kasanga akisalimiana na  Afisa Rasilimali Watu kutoka  Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia lakini pia ni, Mratibu wa dawati la genda Idara ya Utawala na Rasilimali watu Bi.Salome Mziray,mara baada ya kuwasili kwenye   Kituo cha kulelea Watoto yatima cha Nyumba ya Matumaini Miyuji kilichopo Jijini Dodoma katika  maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika leo 08 Machi, 2020.

 Baadhi ya Wanawake kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia wakiwasili katika  Kituo cha kulelea Watoto yatima cha Nyumba ya Matumaini Miyuji kilichopo Jijini Dodoma kwa ajili ya kutoa misaada ya vitu mbalimbali katika  maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika leo Machi 8, 2020.

Afisa Rasilimali Watu kutoka  Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia lakini pia ni, Mratibu wa dawati la genda Idara ya Utawala na Rasilimali watu Bi.Salome Mziray,akiongea na   Msimamizi  wa kituo hicho Sista Anitha Kasanga ambapo leo wametembelea kituo hicho na kutoa misaada ya vitu mbalimbali  katika   Kituo cha kulelea Watoto yatima cha Nyumba ya Matumaini Miyuji kilichopo Jijini Dodoma katika  maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika leo 08 Machi, 2020.

Msimamizi  wa kituo hicho Sista Anitha Kasanga akitoa maelezo mafupi kwa wanawake kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia walipotembelea na kutoa mkono wa faraja kwa Kituo cha kulelea Watoto yatima cha Nyumba ya Matumaini Miyuji kilichopo Jijini Dodoma katika  maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika leo 08 Machi, 2020.

Baadhi ya wanawake kutoka  kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia pamoja na watoto wanaoishi  katika  Kituo hicho , wakiwa wamebeba moja ya mahitaji ambapo wametembelea na kutoa  mkono faraja kwa Kituo cha kulelea Watoto yatima cha Nyumba ya Matumaini Miyuji kilichopo Jijini Dodoma  katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika leo 08 Machi, 2020.

Wanawake kutoka  Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia wakiwa katika picha ya pamoja watoto mara baada ya kutoa mkono faraja kwa Kituo cha kulelea Watoto yatima cha Nyumba ya Matumaini Miyuji kilichopo Jijini Dodoma katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika leo 08 Machi, 2020.

……………………………………………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

Maadhimisho wa siku ya wanawake hufanyika kila mwaka Machi 8 ambapo kila nchi duniani huadhimisha kwa namna yake.

Nchini Tanzania mwaka huu maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika Mkoani Simiyu na yalikuwa na kauli mbiu isemayo Kizazi cha Usawa kwa Maendeleo ya Tanzania ya Sasa na baadae

Watumishi wanawake kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wameungana na wanawake wote duniani kuadhimisha siku hiyo kwa kutembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha Nyumba ya Matumaini Miyuji kilichopo Dodoma na kutoa misaada mbalimbali kwa watoto hao.

Msimamizi  wa kituo hicho Sista Anitha Kasanga amebainisha changamoto katika kituo hicho kuwa ni uhaba wa vitanda vya kulalia Watoto hao na bima za afya kwa ajili ya kuwatibia Watoto hao wanapo ugua.

“Muda wowote tunapokea Watoto wa itikadi yoyote kwani lengo letu ni kuwalea na kuwahudumia Watoto wote bila kubagua, hivyo tunaomba jamii na wadau mbalimbali waendelee kujitokeza kwani umoja ni nguvu”,amesema Sista Kasanga

Kituo cha kulelea watoto cha Nyumba ya Matumaini Miyuji kwa sasa kina jumla ya watoto 63.

Naye mmoja wa Watoto wanaolelewa katika kituo hicho (jina kimeifadhiwa) ametoa neno la shukrani kwa kusema Mungu awabariki sana wanawake kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na watumishi wote ambao hawakuweza kufika.

“Katika  siku hii ya wanawake duniani tumefarijika kwa upendo wenu wa kutukumbuka kwa mahitaji muhimu mlotuletea na Mungu awazidishie mlipo toa “, ameshukuru mtoto huyo.

Kila mwaka 8 Machi wanawake duniani kote huadhimisha siku ya wanawake duniani, ambapo kitaifa yamefanyika  mkoani Simiyu na kwa hapa jijini Dodoma yamefanyika  Shule ya Msingi Mkonze.