Home Mchanganyiko TUNAWAHARIBU WATOTO WA KIUME TUNAJENGA TAIFA GANI: SAMIA

TUNAWAHARIBU WATOTO WA KIUME TUNAJENGA TAIFA GANI: SAMIA

0

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika mkoani Simiyu.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika mkoani Simiyu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa katika Banda la Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati akikagua mabanda katika Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika mkoani Simiyu.

Baadhi ya wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kitaifa yaliyofanyika mkoani Simiyu.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

*****************************

Na Mwandishi Wetu Simiyu

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekemea vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto hasa wakiume ambao wamekuwa wakidhalilishwa kwa kuwaingilia kinyume na maumbile.

Ameyasema hayo leo mkoani Simiyu wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kitaifa mkoani humo.

Amewataka watanzania kusimama pampja kwa kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzie kila mmoja kuwa katika mapambano haya ya kuondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

“Sasa hii tabia ya kuwageuza watoto wa kiume.tumatengeneza taifa gani la kuwaharibu watoto wa kiume na hili haliwapi uhalali kuwafa yia vitendo hivyo watoto wa kike” alisema

Amezitaka Kamati za ulinzi wa Wanawake na watoto kufanya kazi na kuacha kujuana ili Sheria ichukue mkondo wake pale inapotokea mtu amefanya kitendo cha kikatili.

Ameisisitiza jamii kusimama pamoja katika kupinga na kupambana na vitendo vya ukatili katika maeneno yao kwani vitendo vingi hufanywa na watu wa karibu wa familia hivyo kuvifumbia macho na wahanga wa vitendo hivyo kukosa haki zao. 

Naye Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa agemda yabusawa wa kijinsia sio ya wanawake peke yao ila ni ya kwa wote yani wanawake na wanaume ili kuweza kuleta usawa wa kijinsia.

Ameongeza kuwa Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amekuwa chachu kwa watoto wa kike na wanawake wa Tanzania katika kuwaza makubwa katika kuleta mabadiliko katika jamii ya kijinsia.

“Tunamshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwapa fursa wanawake katika uongozi na hakika hatujamuangusha tumezitendea haki nafasi zetu” alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesema kuwa Mkoa utaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu na kuwa na maendeleo kwani mtazamo na elimu itamsaidia mtoto wa kike katika kupambanua mambo na kujiletea maendeleo.

“Tukiweza kumsaidia mtoto wa kike kufika katika maendeleo yake ni kumsaidia kuondokana na changamoto zinazomkwamisha kufikia malengo yake” alisema

Ameongeza kuwa muhimu ni kwa wadau kushirikiana na Serikali kuwezesha mabweni yatakayosaidia watoto wa kike kuondokana na vishawishi vitakavyowasababishia kuwarudisha nyuma katika kufikia ndoto zao.

Mhe. Mtaka amewataka wazazi na walezi kuzingatia elimu ya jinsia kuanzia kazi ya familia ili kuondokana na unyanyasaji wa kijinsia kuanzia katika familia ili kuweza kumkomboa mtoto wa kike na ukandamizaji na unyanyasaji.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake kitaifa yamefanyika katika mkoa wa Simiyu yakiwa na Kauli Mbiu isemayo Kizazi cha Usawa kwa Maendeleo ya Tanzania ya Sasa na Baadaye.