Home Mchanganyiko ZIARA YA MAJALIWA WILAYANI PANGANI

ZIARA YA MAJALIWA WILAYANI PANGANI

0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Bomani Pangani akiwa katika ziara ya mkoa wa Tanga, Machi 6, 2020.

Wananchi wa Pangani wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Bomani Pangani akiwa katika ziara ya mkoa wa Tanga Machi 6, 2020.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa ujenzi wa  ukuta wa mto Pangani kabla ya kuuzindua ukuta huo, Machi 6, 2020. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mussa Sima na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani, Zaibab Abdallah  Issa .

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua  mradi wa ujenzi wa ukuta wa mto Pangani akiwa katika  ziara ya mkoa wa Tanga Machi 6, 2020.  Kulia ni  Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, wa pili kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira, Mussa Sima na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani, Zainab Abdallah. 

Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akitia saini kitabu cha wageni akiwa  kwenye Ofisi ya Mkuu wa polisi wa wilaya ya Pangani, Georgina Matagi (kulia) wakati alipozindua kituo kipya cha  Polisi cha wilaya ya Pangani, Machi 6, 2020. Kituo hicho kimejengwa uhamasishaji uliofanywa na Mkuu wa Polisi wa wilaya hiyo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)