Home Mchanganyiko IGP SIRRO AWATAHADHARISHA WANANCHI WATAKAOVURUGA AMANI YA NCHI

IGP SIRRO AWATAHADHARISHA WANANCHI WATAKAOVURUGA AMANI YA NCHI

0

*************************

04/03/2020 MBULU, MANYARA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amewataka wananchi kuendelea kuimarisha hali ya usalama nchini na kwamba mtu yeyote atakayejaribu kuvuruga amani iliyopo atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria zilizopo.

 

IGP Sirro amesema hayo leo akiwa wilayani Mbulu mkoani Manyara wakati akifungua kituo cha Polisi cha Yaedachini kilichopo wilayani humo ambapo amewataka askari Polisi watakaokuwa wakitoa huduma za kipolisi kwa wateja
kuzingatia weledi na kutenda haki kwa wananchi watakaokuwa wanahudumiwa na kituo hicho kuwa msaada kwao.

 

Aidha, IGP Sirro ameendelea kuwasisitiza wazazi na walezi kuhakikisha wanasimamia malezi kwa watoto wao jambo litakalosaidia kuwaepusha kujiingiza kwenye vitendo vya uhalifu na kuwa kero kwa jamii.

 

Kabla ya kufika wilayani Mbulu, IGP Sirro alikutana na kuzungumza na wananchi wa Dareda na kuwasisitiza kuendelea kutunza amani hasa kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.