Home Siasa DKT. BASHIRU AWASILI MTWARA KWA ZIARA YA KIKAZI

DKT. BASHIRU AWASILI MTWARA KWA ZIARA YA KIKAZI

0

………………………………………………………………………………………………..

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally amewasili Mkoani Mtwara kwa ziara ya siku tatu.

Dkt. Bashiru amewasili asubuhi ya leo tarehe 21 Februari, 2020 uwanja wa ndege wa Mtwara mjini na kupokelewa na mamia ya wanachama, wapenzi na mashabiki wa CCM.

Katibu Mkuu atatembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya za Mtwara Vijijini na Masasi na kuzindua mashina ya wakereketwa wa CCM ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa maagizo ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kuendelea kujenga na kuimarisha Chama katika ngazi za mashina pamoja na kukagua miradi ya maendeleo.