Home Mchanganyiko BALOZI IBUGE AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA KUWAIT NCHINI TANZANIA

BALOZI IBUGE AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA KUWAIT NCHINI TANZANIA

0

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge, akimkaribisha Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Balozi Mubarak Mohammed Alsehaijan leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Balozi Mubarak Mohammed Alsehaijan akimuelezea jambo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge walipokutana
katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge, akimulezea jambo Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Balozi Mubarak Mohammed Alsehaijan leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Balozi Mubarak Mohammed Alsehaijan leo
katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

*****************************

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Balozi Mubarak Mohammed
Alsehaijan katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

 

Pamoja na mambo mengine, mazungumzo hayo yalijadili mambo mbalimbali ikiwemo kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Kuwait kupitia Nyanja mbalimbali ikiwemo uwekezaji wa miradi na biashara pamoja na uundwaji wa tume ya kudumu ya pamoja ya ushirikiano.

 

Aidha, Mhe. Balozi Alsehaijan alitumia fursa hiyo kumkabidhi Katibu Mkuu, Balozi Ibuge salamu za rambirambi kufuatia ajali zilizotokea hapa nchini hivi
karibuni.

 

Kwa upande wake Balozi Ibuge, alimweleza Mhe. Balozi Alsehaijan umuhimu wa kuendeleza jiji la Dodoma na kumkaribisha jijini Dodoma.

 

Mazungumzo hayo yamefanyika siku moja baada ya Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania kusheherejea 59 ya Uhuru wake na miaka 29 ya ukombozi wa taifa hilo yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.