Home Mchanganyiko MRADI WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI WENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI  MILIONI...

MRADI WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI WENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI  MILIONI 800 WAKABIDHIWA KWA WAKULIMA ITIGI

0

Sehemu ya mfereji mkuu wenye urefu wa mita 550, unaotoa maji katika bwawa kubwa  la maji halipo katika picha, na kupeleka mashambani katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji Itagata, Wilayani Itigi Mkoani Singida.

Mhandisi Raphael Laiza, ambaye ni mtaalam mshiriki wa uibuaji na utekelezaji wa mradi kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji akipima mwendokasi wa maji kwenye mfereji mkuu unaopeleka maji mashambani, kwa kutumia kifaa maalum aina ya current meter katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji Itagata wilayani Itigi kabla ya makabidhiano ya mradi huo kwa wakulima mwishoni mwa wiki.

Katika picha ni sehemu ya shamba la mahindi katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji Itagata Wilayani Itigi.

Mhandisi Raphael Laiza, ambaye ni mtaalam mshiriki wa uibuaji na utekelezaji wa mradi kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji akiongea na wakulima kabla ya makabidhiano ya mradi wa kilimo cha umwagiliaji Itagata.

Katika picha Meneja wa Mradi wa Ujenzi wa skimu ya kilimo cha umwagiliaji Itagata  Bw. Steven Daniel akisoma ripoti ya ujenzi wa skimu hiyo.

Katikati aliyeshikilia kifaa cha kupimia mwendokasi na kina na maji katika mfereji mkuu unaopelekea maji mashambani ni Bwana Saidi Luhamla mwenyekiti wa kamati ya kijiji cha Itagata ya Mradi huo wa Umwagiliaji.

Anayesaini hati ya makabidhiano ya mradi  wa Umwagiliaji ni mwakilishi wa wananchi wa kijiji cha Itagata hawapo katika picha.

Katika Picha (kulia) ni Bw, Mussa Shabani katibu wa chama cha Umwagiliaji Itagata na Bw. Andrea Petro katibu wa kamati ya ujenzi wa mradi (kushoto) wakishirikiana kufungua koki ya mfereji mkuu unaotoa maji katika bwawa ili kuruhusu maji hayo kuingia katika mashamba ya wakulima na kuona kama yana mwendokasi wa kutoka kuweza kufika mashambani.

……………………………………………………………………………………………………………..

ASILIMIA 99 YA UJENZI WA MRADI YAKAMILIKA

Na; Mwandishi wetu – Itigi, Singida.

Halmashauri ya Wilaya ya Itigi imekabidhiwa rasmi mradi wa skimu ya kilimo cha Umwagiliaji wenye ukubwa wa eneo la hekta zaidi ya mia moja (100) iliyopo katika kijiji cha Itagata Mkoani Singida tayari kwa ajili ya wakulima na wananchi wa eneo hilo, kutumia kwa shunguli za kilimo kama ajira, kujiongea kipato na uhakika chakula, baada ya ujenzi wa miondombinu ya skimu hiyo kukamilika kwa Asilimia tisini na tisa ( 99%) .

Makabidhiano ya Mradi huo wa Umwagiliaji yalifanyika mwishoni mwa wiki baada zoezi la ukaguzi wa miundombinu ya umwagiliaji ulioshuhudiwa na muwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, wataalam kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Mkandarasi wa Mradi huo MS Fast Construction Company  Ltd Uongozi wa Serikali ya kijiji cha Itagata na wananchi wakulima wa umoja wa umwagiliaji ambao ndiyo watumiaji wakubwa wa mradi huo.

Mradi huo mpya kabisa una ukubwa wa eneo la hekta 120 linalotegemewa kutumika katika kilimo cha umwagiliaji ambapo  jumla ya wakulima zaidi ya mia mbili (200) katika skimu hiyo watapa maeneo kwa ajili ya shughuli za kilimo cha umwagiliaji.

Bwawa kubwa la kuhifadhia maji yatakayotumika katika kilimo lenye ukubwa wa ujazo wa lita milioni moja na laki moja (1,100,000 lts) limejengwa pamoja na mfereji mkubwa wenye urefu wa mita 550 umejengwa sambamba na mifereji mingine midogo  Mitano ya kupela maji mashambani.

Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya wakulima katika kijiji cha Itagata wameishukuru Serikali ya Awamu ya tano  kwa kushirikiana na shirika la maendeleo la kimataifa la Japan JICA kupitia Tume ya taifa ya Umwagiliaji kwa kuwaletea mradi mkubwa wa kilimo cha umwagiliaji, kilimo ambacho hakitegemei msimu wa mvua na kuamini kuwa kitabadilisha maisha yao kwa kiasi kikubwa na kuwa na uhakika wa chakula, Na kuiomba Serikali kuongeza mifereji zaidi ili wakulima waweze kupata maji kirahisi.

Awali akiongea na wakulima hao Mhandisi Raphael Laizer ambaye ni mtaalam mshiriki wa uibuaji na utekelezaji wa mradi huo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,  amewaasa kuilinda na kuitunza miundombinu hiyo ya kilimo cha umwagiliaji, kutumia elimu waliyoipata ya mafunzo na matunzo ya miundombu ya umwagiliaji na kuwa, asilimia moja iliyobakia ya ukamilifu wa ujenzi wa mimndombinu siyo shughuli ya kitaalam bali ni ya udogo ambayo inaweza kukamilika kupitia ada ya mafunzo na matunzo kutoka kwa wakulima wenyewe.

Mradi huo wa kilimo cha umwagiliaji  ambao upo chini ya mradi wa Small Scale Irrigation Development Project (SSIDP) ulianza kujengwa mwezi March mwaka 2017 umekamilika mwaka huu na kukabidhiwa kwa wananchi tayari kwa kuendelea na kilimo cha umwagiliaji ambacho ni kilimo cha uhakika.