Home Mchanganyiko WAHANDISI MKOA TABORA WAPEWA MIEZI MIWILI KUHAKIKISHA WANAPATA LESENI ZINAZOWARUHUSU KUFANYAKAZI

WAHANDISI MKOA TABORA WAPEWA MIEZI MIWILI KUHAKIKISHA WANAPATA LESENI ZINAZOWARUHUSU KUFANYAKAZI

0

Wahandisi kutoka Kanda ya Magharibi na Ziwa wakiapishwa na Rais wa Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET) Mhandisi Menye Maanga wakati wa semina ya siku moja ya utendaji kitaalamu katika fani ya uhandisi kwa Wahandisi ilifanyika leo mkoani Tabora.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa leseni ya kazi kwa Mhandisi kutoka RUWASA  Mpanda Maglalena Mkelemi wakati wa semina ya siku moja ya utendaji kitaalamu katika fani ya uhandisi kwa Wahandisi wa Kanda ya Magharibi na Ziwa.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wahandisi Mhandisi Profesa Ninatubu Lema akitoa hotuba wakati akifungua semina ya siku moja ya utendaji kitaalamu katika fani ya uhandisi kwa Wahandisi wa Kanda ya Magharibi na Ziwa.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akifungua leo semina ya siku moja ya utendaji kitaalamu katika fani ya uhandisi kwa Wahandisi wa Kanda ya Magharibi na Ziwa.

Baadhi ya Wahandisi kutoka Kanda ya Magharibi na Ziwa wakiwa katika semina ya siku moja ya utendaji kitaalamu katika fani ya uhandisi kwa Wahandisi ilifanyika leo mkoani Tabora.

********************************

NA, TIGANYA VINCENT, TABORA.

SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imetoa miezi miwili kwa Wahandisi kuhakikisha wamesajiliwa na kupata leseni za uhandisi zinazotolewa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi nchini (ERB) ili wanapokuwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali waweze kutambulika.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akifungua semina ya siku moja ya utendaji kitaalamu katika fani ya uhandisi kwa Wahandisi wa Kanda ya Magharibi na Ziwa.

Alisema kuwa baada ya kipindi hicho kupita hataki kuona Mhandisi asiye na leseni ya ERB ndani ya Mkoa wa Tabora anafanyakazi.

Mwanri alisema utaratibu wa utoaji wa leseni ni muhimu katika kuhakikisha Wahandisi wanaosimamia miradi wanatambulika na wako tayari katika kuhakikisha usalama wa mazingira na maisha ya wananchi.

Alitoa wito Wahandisi wote ambao hawasijali kuhakikisha watumia nafisi hii ambapo Bodi yao inaendelea kuhuisha leseni ambazo muda wake umekwisha ili ziwe hai na waweze kutekeleza majukumu yao kwa uwazi.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliongeza kuwa waandisi wasipozingatia taaluma zao ni hatari sana kwani majengo yataanguka, madaraja yatabomoka, miundombinu mbalimbali itakuwa hafifu isiyo na ubora hivyo kuleta maafa na hasara kubwa kwa uchumi wa taifa.

Alisema serikali inaendelea kutekeleza miradi mbali mbali ya kimkakati na wasimamizi wa utekelezaji wake ni waandisi hivyo  wanapaswa kuzingatia miiko na maadili ya taaluma za utendaji kazi zao.

Mapema Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Mhandisi Patrick Barozi alisema hadi kufikia sasa kuna jumla ya Wahandisi 3,373 waliopisha na kuna 26,918 ambao wamesajiliwa kufanyakazi nchini.

Alisema kati ya hao 2,700 sawa na asilimia 11 ni wa kike ambapo lengo la Bodi ni kufikia asilimia 50 kwa 50 ndani ya muda mfupi ujao.

Mhandisi Barozi aliongeza Wahandisi wa kike wamekuwa waamiifu wakati wa utekelezaji wa miradi mbalimbali wanayopewa kusimamia na ndio maana Bodi inataka kuongeza idadi yao hapa nchini.

Katika semina hiyo jumla ya Wahandisi 16 wameapishwa na kupatiwa leseni za Bodi.