Home Mchanganyiko BALOZI IBUGE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKUU WA ITIFAKI WA ZIMBABWE

BALOZI IBUGE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKUU WA ITIFAKI WA ZIMBABWE

0

Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Itifaki na Kitengo cha Utafiti, Ofisi ya Rais, Zimbabwe Mhe. Balozi Chipo Zindoga akimueleza jambo Mkuu wa Itifaki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge wakati walipokutana na kufanya mazungumzo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Itifaki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Itifaki na Kitengo cha Utafiti, Ofisi ya Rais, Zimbabwe Mhe. Chipo Zindoga wakati wa mazungumzo baina yao jijini Dar es Salaam

Mkuu wa Itifaki  Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Itifaki na Kitengo cha Utafiti, Ofisi ya Rais, Zimbabwe Mhe. Balozi Chipo Zindoga mara baada ya kukamaliza mazungumzo yao

******************************

Mkuu wa Itifaki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Itifaki na Kitengo cha Utafiti wa Zimbabwe Mhe. Balozi Chipo Zindoga leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine, mazungumzo hayo yalilenga kubadilishana uzoefu wa masuala ya itifaki baina ya Tanzania na ZImbabwe.

Mhe. Zindoga amekuja nchini kujifunza jinsi Tanzania inavyoratibu masuala ya iitifaki ikiwemo kufanikisha kwa mafanikio makubwa ya Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika Mwezi Agosti, 2019 jijini Dar es Salaam.