Home Michezo MTIBWA “HATUPOI” YAIRARUA SIMBA BAO 1:0 MAPINDUZI CUP

MTIBWA “HATUPOI” YAIRARUA SIMBA BAO 1:0 MAPINDUZI CUP

0

******************************

NA EMMANUEL MBATILO

Klabu ya Mtibwa Sugar imefanikiwa kushinda taji la Mapinduzi Cupa baada ya kuichapa klabu ya Simba bao 1:0 katika fainali iliyopigwa katika uwanja wa Amani visiwani Zanzibar.

Mtibwa ilipata bao hilo kupitia kwa nyota wao Awadh Salum mnamo dk.39 na kufanikisha kuisaidia klabu yake kubeba taji hilo.

“Lazima tuwaheshimu wapinzani, kweli kwa upande wao walikuwa wadhaifu lakini kwa upande wangu ilikuwa siku nzuri ya ubora”. Amesema mshambuliaji wa Mtibwa Sugar Jaffary Kibaya.