Home Mchanganyiko TAARIFA YA KUPATIKANA KWA WATOTO WAWILI WALIOPOTEA.

TAARIFA YA KUPATIKANA KWA WATOTO WAWILI WALIOPOTEA.

0

***********************************

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mama mmoja anayefahamika kwa jina la HAWA ALLY @ MKALIPA [40] Mkazi wa Tegeta mkoani Dar es Salaam kwa tuhuma za kupatikana na watoto wawili FAISAL MASHAKA
JUMA, miaka mitano na FARHANA MASHAKA JUMA, mwaka mmoja na miezi mitano walioripotiwa kupotea huko Ituha Jijini Mbeya wakiwa wanacheza jirani na nyumbani kwao.

 

Mtuhumiwa amekamatwa Januari Mosi, 2020 huko Wilayani Nzega Mkoani Tabora baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa za kuwepo kwa mama huyo akiwa na
watoto wawili ambao alisafiri nao hadi mkoani Tabora akitoke hapa mkoani Mbeya.

 

Awali mnamo tarehe 28 Disemba, 2019 majira ya saa 14:00 mchana baba mzazi wa watoto hao MASHAKA JUMA aligundua kupotea kwa watoto wake wawili FAISAL MASHAKA JUMA, miaka mitano na FARHANA MASHAKA
JUMA, mwaka mmoja na miezi mitano wote wakazi wa Shewa Jijini Mbeya.

 

Baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa hizo, lilianza msako mara moja ikiwa ni pamoja na kufanya mawasiliano na mikoa mingine na kufanikiwa kumtia mbaroni
mtuhumiwa akiwa na watoto hao wakiwa hai. Upelelezi wa shauri hili unaendelea.

 

Napenda kuwashukuru wananchi wote, Uongozi wa Serikali Mkoa wa Mbeya, Waandishi wa Habari, Machifu na uongozi wa MUJUTA Mkoa wa Mbeya kwa
ushirikiano wao kwa Jeshi la Polisi katika hatua zote zilizofanikisha kupatikana kwa watoto hao.