Home Mchanganyiko NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, RAMADHANI KAILIMA...

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, RAMADHANI KAILIMA AFANYA ZIARA YA AINA YAKE AKIKAGUA UJENZI WA MAKAZI YA ASKARI, MAKAZI YA IGP NA KUKAGUA UTENDAJI KAZI WA NIDA

0

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Ramadhani Kailima, akisalimiana na baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, kabla ya kukagua ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi hilo ambao unaendelea jijini Dodoma. (PICHA NA VERONICA MWAFISI-MOHA)

Mratibu na Msimamizi Mkuu wa miradi ya ujenzi ambayo
inatekelezwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini
Dodoma, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, SSP Costantine
Kiwone, akimweleza Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima (katikati) na Maofisa wengine hatua mbalimbali za ujenzi wa nyumba za askari, Makao Makuu ya Polisi na makazi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) jijini Dodoma jana. (PICHA NA VERONICA MWAFISI-MOHA)

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Ramadhani Kailima (katikati), akitoa maelekezo kwa Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mbaraka Semwanza (kulia) na Mkurugenzi wa Utawala na Rasirimali Watu, Emmanuel Kayuni (wa pili kulia) baada ya kufanya ukaguzi katika ujenzi wa majengo ya jeshi hilo jijini Dodoma jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Kushughulikia Malalamiko, CP Albert Nyamhanga. (PICHA NA VERONICA MWAFISI-MOHA)

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Ramadhani Kailima (kulia), akiwa na Wakurugenzi na Maofisa wa Wizara hiyo akisisitiza jambo kwa Maofisa wa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Mkoa wa Dodoma, alipofanya ziara ili kuangalia utendaji kazi na huduma zinavyotolewa kwa wananchi. (PICHA NA VERONICA MWAFISI- MOHA)

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Ramadhani Kailima akizungumza na Maofisa wa Jeshi la Polisi baada ya kukagua miradi ya ujenzi inayotekeleza na vyombo vilivyopo chini ya Wizara hiyo zikiwemo nyumba 88 za askari polisi zilizopo Nzuguni, nyumba 30 zilizopo Mashariki, mkoani Dodoma, makazi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) na Makao Makuu ya Polisi. PICHA NA VERONICA MWAFISI- MOHA