Home Michezo MANCHESTER UNITED, EVERTON HAKUNA MBABE

MANCHESTER UNITED, EVERTON HAKUNA MBABE

0

**************************

NA EMMANUEL MBATILO

Kiputepute cha ligi kuu ya Uingerea imeendelea leo, ambapo Manchester United ilikuwa inawakalibisha Everton na kuambulia sare ya mabao 1:1.

Everton ilianza kupata bao la kwanza kupitia kujifunga kwa beki wa kati wa Manchester United Victor Lindelof mnamo dakika 36, na kuwapeleka mbele wakiongoza mpaka mapumziko.

Katika kipindi cha pili timu ya Manchester ilionesha hali ya kuhitaji kusawazisha kwani walikuwa wakipelka mashambulizi kwa timu pinzani hivyo katika mabadiliko waliyoyafanya kipindi cha pili yalizaa matunda.

Manchester United ilifanya mabadiliko kumtoa Jesse Lingard baada ya kupata majeruhi na nafasi yake kuchukuliwa na kinda wa klabu hiyo Mason Greenwood mnamo dakika ya 65.

Greenwood alichukua dakika 12 kuipatia timu yake bao la kusawazisha mnamo dakika ya 77 na kufanya matokeo kuwa sare mpaka mpira ulipomalizika.

Mechi nyingine ilikuwa kati ya Tottenham Spurs wakiwa ugenini kucheza na klabu ya Wolverhampton Wanders na kufanikiwa kutoka kifua mbele kwa mabao 2:1.