*********************
Happy Lazaro,Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewataka wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Arusha kukusanya data za wazazi ambao wameshidwa kutimiza wajibu wao wa kuwasomesha pamoja na kuwahudumia watoto wao ambao wapo chini ya miaka 18.
Aidha pia amewataka wapeleke taarifa zote za matukio ya ambayo yameripotiwa kwenye wilaya zao yanayohusiana na ukatili wa kijinsia ikiwemo idadi ya mashauri yaliyopelekwa mahakamani ,na mangapi hayajapelekwa pamoja na vikwazo vilivyopo ili viweze kufanyia kazi kwa haraka.
Ameyasema haya jana kwenye kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa mkoa Wa Arusha yaliongozwa na maandamano ya jeshi la Polisi na kuhitimishwa katika hospital ya rufaa ya mkoa Wa Arusha (mount Meru) ambayo yamebeba kauli mbiu ya “Kizazi chenye usawa simama dhidi ya ubakaji”.
” tutachukuwa taarifa zote tutakazo zibaini na tutachunguza kama changamoto zipo katika mahakamani zetu , Polisi , au kwa wataalamu wetu wa wa afya ambao wanatakiwa kutoa taarifa rasmi ya ripoti ya kitaalamu ya kuthibitisha kama kweli kuna mtu amefanyiwa ukatili wa kijinsia ili iwe kama ushaidi wa kumpeleka mhalifu mahakamani tukiwa na ushaidi wa kutosha na tunasema sisi kama mkoa wa Arusha tumeanza kazi ya kuwasaka na kuwachukulia hatua wale wote wanaofanya matukio ya ukatili wa kijinsia”amesema Gambo.
Amebainisha kuwa taarifa inaonyesha kadri Siku sinavyoenda matukio ya ukatili Wa kijinsia yanapungua lakini taarifa,mwitikio na twasira inaonyesha matukio ya ukatili Wa kijinsia yapo ,na hii inatokana uwezekano Wa baadhi ya matukio kutoripotiwa katika sehemu husika au baadhi ya wananchi wamekata tamaa baada ya kuona matukio wanayoripoti hayafiki katika hatua ambayo waowanategemea.
Kamanda wa Polisi mkoa Wa Arusha Jonathan Shana amesema wao kama kama jeshi la Polisi wameshaanza Kazi rasmi ya kuwadhibiti watu wanaofanya matendo ya ukatili wa kijinsia na wanaanza rasmi kuwasaka popote pale walipo na watawachukulia hatua kali za kisheria hivyo aliwasihi wananchi watii sheria bila shuruti , na kuwaambia kuwa mapambano ya kupinga ukatili wa kijinsia ni wa kila mtu awe mwanaume au mwanamke.
Naye Mganga mfawidhi wa hospital ya rufaa ya mount Meru Shafii Msechu amesema kuwa ,kwa mwaka huu wamepokea wahanga Waliofanyiwa ukatili Wa kijinsia 333,huku waliopelekwa mahakamani 10 kesi zilizopelekwa mahakamani zikiwa ni 9 na wanahakikisha wahalifu wanachukuliwa hatua.
Amesema kuwa,wananchi wamekuwa hawajitokezi kutoa taarifa za namna wanavyofanyiwa ukatili huo wengi wao wakiwa wanaogopa kuonekana kitu ambacho kinawanyima haki yao.
Kamishna msaidizi wa polisi ambaye pia ni Mwenyekiti wa mtandao wa Polisi wanawake mkoa Wa Arusha (TPF-NET) Mary Kipesha amesema kuwa matukio ya ukatili Wa kijinsia yamepungua sana kwa mwaka huu tofauti na mwaka Jana ambapo Kwa kipindi cha mwaka 2018 kesi za ukatili Wa kijinsia ziliripotiwa 161 huku mwaka huu 2019 January hadi December zikiwa zimeripotiwa kesi 89 ambapo kunaupungufu Wa asilimia 32.5%.
Amesema kuwa ,kwa upande wa kesi za kulawiti mwaka Jana 2018 zilikuwa 62 huku mwaka huu 2019 kwa kipindi cha January hadi Decemba zikiwa na kesi 52 ambapo kuna upungufu wa asilimia 7.9% na hii inaonyesha wamepata mafanikio makubwa mno ya kupunguza uhalifu wa unyanyasaji wa kijinsia .
Hivyo katika kuhakikisha swala hilo linaisha wanaendelea kutoa Elimu kwa wanafunzi wa mashuleni, vyuoni pamoja na wananchi kwa ujumla .