Home Mchanganyiko MHOGO KUTUMIKA KATIKA MATUMIZI MBALIMBALI NJE YA CHAKULA

MHOGO KUTUMIKA KATIKA MATUMIZI MBALIMBALI NJE YA CHAKULA

0

**************************************

NA EMMANUEL MBATILO

Vijana kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, (UDSM) wameamua kujikusanya pamoja na kutengeneza kampuni ya JV Biotech Interprises limited ambayo inahusiana na kuutengeneza Muhogo kuwa na matumizi mbalimbali nje ya Chakula.

Akizungumza katika Maonesho ya Biashara katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam,Bi.Aikael Felix amesema kuwa waliamua kujihusisha na kubadilisha thamani ya Muhogo yaani usizoeleke kutumika kama chakula bali unaweza kutumika kama chakula cha mifugo, dawa na mbolea ambayo ni nzuri katika matumizi ya bustani nyumbani kwani mara nyingi mbolea hiyo haichanganywi na kemikali ya aina yoyote.

“Kiwanda kipo Kiwangwa wilayani Bagamoyo pia tuna ofisi pale Riverside pamoja na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM)”. Amesema Bi.Aikael.

Aidha Bi.Aikael amesema kuwa mpaka sasa wamefanikiwa kuanzisha shamba la mihogo la hekali 50 na kutoa ajira kwa wakulima wa mihogo.

Pamoja na hayo Bi. Aikael amesema kuwa malengo yao ni kuyafikia masoko ya nje ya nchi ili kuweza kutangaza bidhaa zao zitokanazo na zao la mihogo.