Home Mchanganyiko NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI ZASHAURIWA KUCHUKUA TAHADHARI MAGONJWA YA MILIPUKO

NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI ZASHAURIWA KUCHUKUA TAHADHARI MAGONJWA YA MILIPUKO

0

Naibu waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki,Dokta Damas Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhairishwa kwa bunge la Afrika Mashariki Jana.

…………….

Happy Lazaro,Arusha.

Nchi za jumuiya ya  Afrika mashariki zimeshauriwa kuchukua tahadhari ya pamoja namna ya kudhibiti  magonjwa ya milipuko katika maeneo ya mipakani.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wa pili na kikao cha tatu na bunge la nne la jumuiya ya Afrika Mashariki,Naibu Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Dokta Damas Ndumbaro amesema kuwa,nchi za Afrika mashariki kwa pamoja zinapaswa kuangalia utimamu wao na utayari wao katika vituo vya mipakani katika  kudhibiti magonjwa ya milipuko  .

Dokta Ndumbaro amesema kuwa,pamoja na kuwepo kwa soko la pamoja la jumuiya ya Afrika  mashariki ambalo linaruhusu watu kutembea kwenda sehemu moja kwenda  nyingine ,pamoja na kuwa hilo limewekwa kwa nia nzuri ,lakini hilo linaweza kuwa ndio chanzo na sababu ya kusababisha mlipuko ya magonjwa hayo ,hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha  tunachukua tahadhari ya magonjwa hayo mapema.

“ni lazima sisi kama nchi za EAC tuhakikishe tunaungana pamoja na kuweka nguvu zetu katika kuhakikisha tunadhibiti milipuko ya magonjwa ili nchi zetu ziendelee kubaki salama.”amesema.

Amesema kuwa,katika kikao hicho cha bunge kwa pamoja wameweza kuzungumzia maswala ya kuimarisha maabara zetu ili kuweza kugundua watu wenye ugonjwa huo haraka iwezekanavyo .

“pia tumeweza kujadili kwa kina maswala ya chanjo mbalimbali na umuhimu wa hizo chanzo katika kuwakinga watoa huduma ambao wanakuwa mstari wa mbele kabisa katika kuzuia kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa huo,na kwa kujiwekea mikakati hii tunaweza kwa kiasi kikubwa sana kudhibiti magonjwa hayo .”amesema Dokta Ndumbaro.

Naye Mbunge wa jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka nchini Kenya ,Abdulkadir  Mohamed amesema kuwa,wananchi wengi  katika nchi za jumuiya wameshaelimishwa juu ya magonjwa hayo na namna ya kuchukua tahadhari pindi watakapoona viasharia vya magonjwa hayo .

Aidha alizitaka nchi za Afrika mashariki kufanya kazi kwa pamoja katika kusaidiana  na kuwataka wasilale  kabisa bali waunganishe nguvu pamoja katika kudhibiti magonjwa hayo.

” napenda kuwahakikishia wageni wanaokuja nchi za Afrika mashariki kuwa wasiogope bali nchi zetu zipo  salama kwani serikali zetu zimeweka utaratibu wa kutosha wa kupambana na magonjwa hayo katika kukagua watu na kujua kabla tukio hilo halijatokea maeneo mbalimbali hivyo nawatangazia kabisa nchi zetu zipo salama hakuna Ebola.”amesema Mohamed.

Amesema kuwa,katika viwanja vyote vya ndege wameweka mikakati kamili na utayarishi wa kupambana na magonjwa  hayo  ikiwa bahati mbaya tukio litatokea