Home Mchanganyiko AJALI YA MAGARI MAWILI KUGONGANA NA KUSABABISHA VIFO NA UHARIBIFU MKOANI MBEYA

AJALI YA MAGARI MAWILI KUGONGANA NA KUSABABISHA VIFO NA UHARIBIFU MKOANI MBEYA

0

*******************************

Mnamo tarehe 03.12.2019 majira ya saa 10:00 asubuhi huko eneo la Kanyegele
@ Airport lililopo Kijiji cha Ibula, Kata ya Kiwira, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya
Rungwe, Mkoa wa Mbeya. Gari yenye namba ya usajili T257 CZA aina ya
HOWO ikiwa na tela yenye namba ya usajili.T.597 CRR mali ya Kampuni ya
Camel Oil ya Dar es Salaam ikiwa inatokea Mbeya kwenda Malawi kupeleka
mafuta ya diesel, ilifeli breki na kugonga gari nyingine T.840 CLY aina ya Canter
mali ya Rungwe Spring Water na kusababisha vifo vya watu watatu ambao ni:-

1. FRANK SAMWEL SAGUMO @ CHOTA [48] dereva wa tanker, mkazi wa
Morogoro.
2. Ametambulika kwa jina moja la SILAS ambaye ni utingo wa Tanker, mkazi wa
Morogoro.
3. NELSON SAMSON [35] dereva wa gari ya kampuni ya maji ya Rungwe
Spring na mkazi wa Airport Mbeya.

Aidha katika ajali hiyo kumetokea uharibifu wa magari yote mawili pamoja na
kumwagika kwa mafuta aina ya diesel. Chanzo cha ajali ni hitilafu kwenye mfumo wa breki wa gari Tanker la mafuta na kupelekea tairi moja la nyuma kushika moto.

Miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Rungwe – Makandana.