Home Mchanganyiko NAIBU WAZIRI SIMA AAGIZA BARAZA LA MAZINGIRA KUPITIA UPYA VIBALI VYA KUFANYA...

NAIBU WAZIRI SIMA AAGIZA BARAZA LA MAZINGIRA KUPITIA UPYA VIBALI VYA KUFANYA SHUGHULI YA UWEKEZAJI KATIKA UFUKWE WA FERI MKOANI MTWARA

0

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima (kushoto) akizungumza akiwa katika ziara eneo la ufukwe mjini Mtwara alipofanya ziara na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC). Katika ni Mwenyekiti wa Bodi ya NEMC Prof. Esnat Chagu.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Prof. Esnat Chagu, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Samuel Gwamaka na Meneja wa NEMC Kanda ya Kusini Jamal Baruti.

Viongozi wakiwa katika ziara katika ufukwe ambao mwekekezaji amekutwa akifanya shughuli eneo la feri mjini Mtwara.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Prof. Esnat Chagu wakimsikiliza mwekezaji Chandra Shekhar wa kiwanda cha Alpha Krust katika ufukwe mjini Mtwara walipofanya ziara eneo hilo.

…………………………………………….

Na Robert Hokororo, Mtwara

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima amelielekeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kupitia upya vibali vya kufanya shughuli ya uwekezaji katika ufukwe wa bahari eneo la Feri mkoani Mtwara.

Sima ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara yake pamoja na NEMC kwenye mikoa ya kusini ya Lindi na Mtwara kuona namna shughuli za uhifadhi wa mazingira zinavyotekelezwa.

Akitoa maelekezo hayo kuhusu mwekezaji Chandra Shekhar wa kiwanda cha Alpha Krust alitaka NEMC ianze kupitia upya nyaraka ambazo aliombea vibali vya kufanya shughuli hizo katika eneo hilo.

Aidha, alisema baada ya kumsikiliza akidai alipewa vibali kuna haja sasa ya kumhakiki ili aweze kupewa cheti ya mazingira kama atakuwa amefuata sheria za mazingira.

Naibu waziri pia aliagiza uangaliwe upya mpango wa matumizi ya ardhi katika eneo hilo kuwa yamepangwa yatumikaje ili kama yako sahihi basi apate cheti cha kuendelea na shughuli zake.

“Watu wengu wamekuwa wakiwekeza katika maeneo ya fukwe bila utaratibu na kufanya uharibifu wa mazingira lakini sisi jukumu letu ni kulinda fukwe hizi na ambazo pia ni vyanzo vya sasa kama hatujalinda tutapoteza rasilimali hii ya bahari, hivyo nasitisha kwanza shughuli za mwekezaji huyu hadi pale NEMC watakapofanya review ya vibali vyake,” alisema.

Naibu waziri aliongeza kuwa Sheria ya Mazingira yam waka 2004 57 (2) inampa waziri dhamana ya kuamua ndani ya mita 60 pembezoni mwa bahari nini kifanyike kuendana na mazingira ya eneo hilo lakini si kila shughuli anaweza kuruhusu kufanyika.