Na Mwandishi Wetu.
TANZANIA Bara itacheza na Uganda katika Nusu ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Wanawake Jumamosi Saa 10: 00 jioni Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Nusu Fanal nyingine ya michuano hiyo ya tatu ya CECAFA Challenge kwa kubwa upande wa wanawake itatangulia Saa 8:00 mchana kati ya Burundi na Kenya hapo hapo Azam Complex, Jumamosi.
Fainali ya michuano hiyo itafanyika Jumatatu Saa 10:00 jioni ikitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu. 

Kilimanjaro Queens imetinga Nusu Fainali baada ya kuongoza Kundi A kufuatia kushinda mechi zake zote za kundi hilo, ikiichapa 7-0 Zanzibar, 9-0 Sudan Kusini na 5-0 Burundi katika mechi zake tatu za mwanzo hivyo kuongoza kundi hilo kwa pointi zake tisa na mabao 20 ya kufunga, ikiwa haijafungwa hata bao moja hivyo kwenda Nusu Fainali kibabe.